CHAUKIDU

Hello all!
Thanks for visiting CHAUKIDU’s website. This is a free blog for comments, questions and/or any concerns. Please feel free to contribute on any issues that need response from the web admins, the President, Director, Board Members or any other member.┬áNOTE: All comments will have to be approved before they can appear on the blog.

Karibuni (welcome)!


Comments

CHAUKIDU — 11 Comments

 1. Hello everyone!!

  This is Chaukidu blog. Please feel free to contribute on any issues warranting your attention. NOTE: All comments will have to be approved before they can appear on the blog. Thank you for visiting Chaukidu Blog.

 2. Kwanza namshukuru sana Patrick Mose kwa juhudi zake za kukarabati tovuti hii ya CHAUKIDU. Hongera sana. Pili nimeulizwa swali na baadhi ya wakereketwa wa Kiswahili na kushindwa jinsi ya kuwajibu. Wanauliza nini hasa maana ya neno “hamirojo”? Kamusi moja yasema ni “chakula cha protini” nayo nyingine inasema “chakula cha wanga.” Basi kweli i wapi?

 3. Natumia nafasi hii kuwashukuru nyote ambao umechangia na mnaendelea kufanya kazi bora kwa kuinua Kiswahili. Nawapongezeni na kuwapa nguvu kwamba, nawaonea fahari, kazi hii inapendeza na inatia matumaini…najivunia…

 4. Hamjambo wana CHAUKIDU,

  Mimi ni Meneja wa Mradi wa Swahilihub.com tovuti inayoendeshwa na gazeti la Taifa Leo, Mwananchi, Mwanaspoti , QTV, Qfm na NTV- vyote vyombo vya habari vya Kiswahili vya Kampuni ya Nationa Media Group vilivyo Kenya na Tanzania.

  Tunawezaje kushirikiana na sisi.
  Hivi karibuni tunaanzisha jarida la Kiswahili la mtandaoni tukishirikiana na Chuo CHa Kenyatta hapa Nairobi na tunaandaa kanzi nzito ya iksiri za MA, PhD, na DPhil zote za Kiswahili na tafiti nyingine zilizowahi kufanyika katika Kiswahili kutoka vyuo vyote vifundishavyo Kiswahili ulimwenguni.
  Pia kuna video, makala , mashairi na habari kwenye tovuti ya http://www.swahilihub.com.
  Tuwasiliane.

  Shukran,

  Regards,
  Hezekiel Gikambi,
  Project Manager- SWAHILIHUB,
  Nation Media Group
  Mobile: +254 722 358 448/+254786950509.
  E-mail: hgikambi@ke.nationmedia.com
  hezekielgikambi@gmail.com
  Office +254 719038424,+254 203288424.
  http://www.swahilihub.com
  Nation Centre, 3th floor, Kimathi Street Nairobi, Kenya.

 5. Habari zenu.
  Bila shaka hamjambo.
  Mimi nina maswali mawili tu na pendekezo. Kwanini blogu hii ni ya Chama cha Ukuzaji Kiswahili Duniani lakini jambo la kustaajabisha karibu kila jambo humu limeandikwa kwa Kiingereza,mi naona ajabu kuliko hata neno lenyewe ajabu. Nafikiri blogu hii ingekuwa kwa lugha hizo mbili basi lakini mwonekano wa msingi ukawa kwa Kiswahili, atayetaka Kiingereza kama ni lazima sana akabadili lugha na kuona kwa lugha atakayo. Tunataka kukuza Kiswahili ambacho hata sisi hatukitumii,nilikuwa natembelea mtandao huu nikiwa na rafiki yangu kutoka Italia hakika amebaki kinywa wazi maana hata yeye hakutegemea kukuta Kiingereza.
  Jambo la pili,ni kwanini isitengenezwe njia rahisi ambayo kila mdau angeweza kujiunga na wadau wengine wa Kiswahili,kama vile njia ya makundi ya mitandao kama whatsapp japo huu huchukua watu wachache sana,basi telegram ambao kundi huweza kuchukua idadi kubwa sana ya watu. Ni maoni tu kuona kama inafaa.

  • Habari gani Kimaro?
   Tunashukuru kuwa umepata fursa ya kutembelea ukurasa wetu. Hata hivyo tumeshindwa kuelewa ni kwanini wewe, pamoja na rafiki yako wa Italia mlishindwa kuona kuwa tovuti yetu ina kurasa pacha, za Kiswahili na Kiingereza. Tafadhali nenda kwenye menyu yetu ya Kiswahili na ufurahie urari wa taarifa zetu katika lugha hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *