2016 Nairobi

Kongamano la Kimataifa la Chaukidu

Nairobi, Kenya

Hisani huanzia nyumbani! Chaukidu kingependa kutangaza kuwa kitakuwa na kongamano la kwanza katika eneo la Afrika Mashariki kikishirikiana na Chuo Kikuu cha Katoliki cha Afrika Mashariki, CHAKAMA na CHAKITA. Mada kuu ni “Taaluma za Kiswahili Karne ya 21 Nyumbani na Ughaibuni: Tutokako, Tulipo, na Tuendako!” Walengwa wakuu wa kongamano ni wanataaluma na wadau wa Kiswahili katika Afrika Mashariki, Afrika na dunia kwa ujumla. 

MahaliChuo Kikuu Katoliki cha Afrika Mashariki, Nairobi
TareheDisemba 16  - 17, 2016 (Ijumaa/Jumamosi).
KufikaAlhamisi Disemba 15, 2016.
IkisiriJuni 20, 2016
MajibuJulai 11, 2016
Miswada Septemba 30, 2016

Tafadhali wasilisha ikisiri yako katika muda uliopangwa. Tuma ikisiri yako kwa: chaukidu2016nairobiconference@gmail.com

Kupata maelezo zaidi kuhusu kongamano hili, chagua katika menyu iliyoko upande wa kushoto wa ukurasa huu