Chaukidu 2017

Kongamano la Chaukidu 2017

Kongamano la kila mwaka la sita la Chaukidu limepangwa kufanyika kuanzia tarehe 21 hadi 23 Aprili, 2017, katika hoteli ya Holiday Inn, iliyoko katika anuani hii: Schaumburg Area 3405 Algonquin Road, Rolling Meadows, IL 60008, USA.

Kwa mara ya nyingine tangu kuanzishwa kwa Chaukidu, kongamano litawaleta wazungumzaji wazawa wa Kiswahili wenye asili ya Tanzania, Kenya, Uganda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na nchi nyingine za Afrika Mashariki na Kati, ambao wanaishi katika maeneo ya Chicago na Marekani kwa ujumla. Kwa taarifa zaidi kuhusiana na kongamano hili, tafadhali tembelea tovuti yetu mara kwa mara. Maelekezo zaidi yatakufikieni mapema iwezekanavyo.