Dar es Salaam 2017

Kongamano la Kimataifa la 3 la Chaukidu

Disemba 15 - 16, 2017 Dar es Salaam, Tanzania

Mwenye macho haaimbiwi tazama! Chaukidu kingependa kutangaza la tatu la kimataifa na la pili katika eneo la Afrika Mashariki litakalofanyika katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, jijini Dar es Salaam, Tanzania. Kongamano hili linaletwa kwenu kwa kushirikiana na Taasisi ya Taaluma za Kiswahili (TATAKI) ya Chuo Kukuu cha Dar es Salaam. Mada kuu ni “Dira ya Karne ya 21– Ukuaji wa Kiswahili na Ustawi wa Jamii” Walengwa wakuu wa kongamano ni wanataaluma, wadau na wazungumzaji wa Kiswahili katika Afrika Mashariki, Afrika na dunia kwa ujumla. 

MahaliChuo Kikuu cha Dar es Salaam
TareheDisemba 15  - 16, 2017 (Ijumaa/Jumamosi).
KufikaAlhamisi Disemba 14, 2017.
IkisiriJuni 19, 2017
MajibuJulai 21, 2017
Miswada Oktoba 30, 2017

 

Tafadhali wasilisha ikisiri yako katika muda uliopangwa. Kupata maelezo zaidi kuhusu kongamano hili, chagua katika menyu iliyoko upande wa kushoto wa ukurasa huu.

Ikiwa ungependa kuchangia kongamano hili, basi unakaribishwa kufanya hivyo. Tuna idadi kubwa ya wanafunzi wa uzamivu na uzamili ambao wangependa kuhudhuria kongamano hili ila wanashindwa kwa sababu ya gharama kubwa. Mchango wako utasaidia kuwafadhili wanafunzi hawa, hasa kwa malazi. Kwa kuchangia, tafadhali tumia kitufe kilichopo hapo chini.

Toa Mchango Wako Hapa