Dar-Hoteli

Taarifa za awali za hoteli

Kamati ya Maandalizi imefanya mazungumzo na Hoteli ya Fahari, iliyoko karibu na Mlimani City Mall, na watatoa vyumba 18 kwa gharama ya TSH 50,000 badala ya $30 hadi $40. Kutokana na uchache wa vyumba vilivyotolewa kwa bei hiyo, kipaumbele kitatolewa kwa wale wanaotoka nje ya Dar es Salaam, na kwa wale watakaowahi kutoa taarifa. Kama unahitaji kupata mojawapo ya nafasi hizi, tafadhali wasiliana na Rais wa Chaukidu, Dkt. Mahiri Mwita, kabla ya Disemba 5.

Vilevile zipo hoteli nyingine zilizoko karibu na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambazo kamati inazipendekeza kwa wale wote wanaohitaji huduma hiyo. Hoteli hizo ni pamoja na Wistas Inn na Blue Bird. Gharama ya hoteli hizi itakuwa ni Tsh 60,000 kwa Watanzania na $60 kwa wasio Watanzania.