Mada Nairobi 2016

Mada/Majopo ya Kongamano la Nairobi

 1. Ukuaji na ukuzaji wa Kiswahili kuwa taaluma ya kiakademia yenye kina na mbinu zake za utafiti (kama taaluma nyinginezo za kisayansi, sayansi-jamii na sanaa-jamii)
 2. Ufundishaji wa Kiswahili kama lugha ya kigeni
 3. Ufundishaji wa Kiswahili nyumbani (elimu ya msingi, sekondari, na katika vyuo)
 4. Kiswahili na/katika vyombo vya habari
 5. Kiswahili na mitandao ya kijamii (blogu, Facebook, twitter, WhatsApp, n.k.)
 6. Fasihi ya Kiswahili (riwaya, tamthlia, ushairi)
 7. Kiswahili na muziki (wa dansi, Taarabu, kizazi kipya, n.k.)
 8. Kiswahili na sanaa za maigizo (michezo ya redioni, runingani, filamu, n.k.)
 9. Vibonzo vya Kiswahili
 10. Kiswahili na ukuaji au udororaji wa demokrasia
 11. Nafasi ya Kiswahili katika kukuza uchumi wa Afrika Mashariki
 12. Nafasi ya Kiswahili katika kuimarisha au kudhoofisha jumuiya ya Afrika ya Mashariki
 13. Nafasi ya Kiswahili katika kupanua ajira kwa vijana
 14. Utafiti na machapisho ya Kiswahili katika tanzu zake mbalimbali – isimu, lugha, fasihi, n.k.
 15. Mchango wa Kiswahili katika kukuza au kuua lugha za jamii ndogondogo
 16. Mchango wa Kiswahili katika kukuza au kuathiri Kiingereza
 17. Kiswahili na huduma za kijamii
 18. Leksikolojia na leksikografia ya Kiswahili
 19. Ufasiri na ukalimani
 20. Katiba na sheria
 21. Kiswahili mitaani (matumizi halisi) na chuoni (utafiti, ufundishaji, n.k.)
 22. Mwanafunzi wa Kiswahili: ufundishaji wa darasani ughaibuni na programu za uzamivu nyumbani
 23. Usanifishaji na uhurishaji
 24. Lahaja zinazoibukia: KiSheng, KiSwanglish, n.k.
 25. Hali ya Kiswahili nchini Rwanda, Burundi, DRC na Uganda
 26. Kusambaa kwa Kiswahili nje ya bara la Afrika
 27. Ushirikiano wa wataalamu wa Afrika Mashariki na wa ughaibuni katika utayarishaji wa matini za kufundishia Kiswahili kama lugha ya kigeni
 28. Nafasi ya teknolojia katika ufundishaji wa Kiswahili
 29. Mbinu na mikakati mipya/ibuka za kufundisha na kujifunza Kiswahili
 30. Utamaduni wa Waswahili/Kiswahili
 31. Tathmini na utahini wa Kiswahili katika madarasa ya Kiswahili kama lugha ya kigeni na kama lugha ya pili (nyumbani)
 32. Mitihani ya kutathmini uwezo wa wanafunzi wa lugha ya Kiswahili kama lugha ya kigeni