MASKANI

Dr. Mahiri Mwita
Rais

Hamjambo wakereketwa wote wa Kiswahili! Kwa niaba ya wanachama wote wa CHAUKIDU, natoa shukrani za dhati kwa kutembelea tovuti ya Chama cha Ukuzaji wa Kiswahili Duniani (CHAUKIDU).Tunayo furaha kubwa  kuwatangazia wakereketwa wote wa Kiswahili po pote pale mlipo ulimwenguni kwamba tumeunda chama hiki kwa madhumuni ya kuikuza lugha ya Kiswahili na utamaduni wake Ulimwenguni. Chama hiki si kwa Waswahili peke yao bali kwa wakereketwa wa Kiswahili wanaofundisha Kiswahili, watafiti, wanafunzi, waandishi wa habari, wasanii mbalimbali, waandishi wa vitabu vya Kiswahili pamoja na wachapishaji, wahudumu wa utalii katika nchi zinazotumia Kiswahili, na sehemu mbalimbali za kazi kama vile mashule, vyuo vya elimu, teknolojia, au biashara, hasa wale wenye uhusiano wa kitaifa au kimataifa na nchi zinazotumia Kiswahili. Chama hiki kitawafaidi wale wote wanaojihusisha kwa hali yo yote ile na Kiswahili, wadau wa Kiswahili, na wale wote wanaoithamini lugha ya Kiswahili na utamaduni wake, na wasemaji wa Kiswahili kwa ujumla. Hizi ni habari njema, sivyo? Tafadhali jiunge nasi na wapashe wengine habari ili kuifanya jumuiya yetu kukua na kuwa kubwa zaidi. Asante sana na karibu sana!

Taarifa Nyingine