Uanachama

Mpenzi mwanachama mtarajiwa,

Tunayo furaha kukuletea mwaliko huu wa kujiunga na jumuiya ya Chaukidu, chama kisichokuwa na malengo ya kupata faida za kifedha. Kama mmoja wa watu wenye (au watarajiao kuwa na) mahusiano na Afrika ya Mashariki, lugha ya Kiswahili na utamaduni wake, tunaamini jumuiya hii itakunufaisha. Vilevile tunaamini kuwa utaifaidisha pia jumuiya hii kwa mawazo yako na uanachama wako. Kwa hiyo, uanachama wako utakuwa ni hatua muhimu sana ya kutuwezesha kufikia moja ya malengo yetu – kuwapa watu wote duniani fursa ya kujiunga na jumuiya yenye umuhimu mkubwa.

Ada yetu kwa wanachama wapya kutoka katika dayaspora (wale waishio nje ya Afrika Mashariki) ni kidogo tu – $30 kwa uanachama wa kawaida, na $15 kwa wanafunzi wasomao katika taasisi mbalimbali katika dayaspora. Uanachama wa kawaida kwa waishio Afrika ya MAshariki ni $20 na kwa wanafunzi waishio Afrika ya Mashariki ni $5 tu.

Kujiunga na chama hiki, tafadhali jaza na tuma kwa mwakilishi wa Chaukidu aliye karibu nawe, au uitume kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Chaukidu Prof. Leonard Muaka, Department of World Languages and Cultures, Locke Hall, Room 350, 2441 Sixth Street, NW Washington, DC 20059.

Kama una swali lolote, tafadhali usisite kuwasiliana na Mkurugenzi Mtendaji kupitia lemuaka@gmail.com au Rais Dkt. Mahiri Mwita kupitia mwita@princeton.edu. Unaweza pia kujaza fomu iliyoambatanishwa hapa na kulipa kwa kutumia Paypal hapo chini.

Tunayo furaha kuwa tupo hapa kwa ajili yako, na kwamba tutafanya kazi hii kwa pamoja.

 

 

Please submit your payment using the Paypal submit button below  


Annual Membership – CHAUKIDUComments

Uanachama — 1 Comment