Hello all! Thanks for visiting CHAUKIDU’s website. This is a free blog for comments, questions and/or any concerns. Please feel free to contribute on any issues that need response from the web admins, the President, Director, Board Members or any other member. NOTE: All comments will have to be approved before they can appear on the blog.
Karibuni (welcome)!
Ken Walibora
Kwanza namshukuru sana Patrick Mose kwa juhudi zake za kukarabati tovuti hii ya CHAUKIDU. Hongera sana. Pili nimeulizwa swali na baadhi ya wakereketwa wa Kiswahili na kushindwa jinsi ya kuwajibu. Wanauliza nini hasa maana ya neno “hamirojo”? Kamusi moja yasema ni “chakula cha protini” nayo nyingine inasema “chakula cha wanga.” Basi kweli i wapi?
Siraj Salum
maana sahihi ya “HAMIROJO” ni chakula cha wanga
Judith
Natumia nafasi hii kuwashukuru nyote ambao umechangia na mnaendelea kufanya kazi bora kwa kuinua Kiswahili. Nawapongezeni na kuwapa nguvu kwamba, nawaonea fahari, kazi hii inapendeza na inatia matumaini…najivunia…
Leonce Rushubirwa
Website ni nzuri. Asante watengenezaji. Ujuzi wenu tunauona.
Amiri S
Ipi ni ni sahihi?
Swahili language Au Kiswahili languaje
Hezekiel Gikambi
Hamjambo wana CHAUKIDU,
Mimi ni Meneja wa Mradi wa Swahilihub.com tovuti inayoendeshwa na gazeti la Taifa Leo, Mwananchi, Mwanaspoti , QTV, Qfm na NTV- vyote vyombo vya habari vya Kiswahili vya Kampuni ya Nationa Media Group vilivyo Kenya na Tanzania.
Tunawezaje kushirikiana na sisi.
Hivi karibuni tunaanzisha jarida la Kiswahili la mtandaoni tukishirikiana na Chuo CHa Kenyatta hapa Nairobi na tunaandaa kanzi nzito ya iksiri za MA, PhD, na DPhil zote za Kiswahili na tafiti nyingine zilizowahi kufanyika katika Kiswahili kutoka vyuo vyote vifundishavyo Kiswahili ulimwenguni.
Pia kuna video, makala , mashairi na habari kwenye tovuti ya http://www.swahilihub.com.
Tuwasiliane.
Shukran,
Regards,
Hezekiel Gikambi,
Project Manager- SWAHILIHUB,
Nation Media Group
Mobile: +254 722 358 448/+254786950509.
E-mail: hgikambi@ke.nationmedia.com
hezekielgikambi@gmail.com
Office +254 719038424,+254 203288424.
http://www.swahilihub.com
Nation Centre, 3th floor, Kimathi Street Nairobi, Kenya.
Hezekiel Gikambi
http://www.swahilihub.com imejengwa kuwa ‘Kitovu cha Kiswahili’ kama kauli mbiu yake isemavyo.
Hezekiel Gikambi
Mawazo na maoni yenu zaidi yanakaribishwa.
Living Kimaro
Habari zenu.
Bila shaka hamjambo.
Mimi nina maswali mawili tu na pendekezo. Kwanini blogu hii ni ya Chama cha Ukuzaji Kiswahili Duniani lakini jambo la kustaajabisha karibu kila jambo humu limeandikwa kwa Kiingereza,mi naona ajabu kuliko hata neno lenyewe ajabu. Nafikiri blogu hii ingekuwa kwa lugha hizo mbili basi lakini mwonekano wa msingi ukawa kwa Kiswahili, atayetaka Kiingereza kama ni lazima sana akabadili lugha na kuona kwa lugha atakayo. Tunataka kukuza Kiswahili ambacho hata sisi hatukitumii,nilikuwa natembelea mtandao huu nikiwa na rafiki yangu kutoka Italia hakika amebaki kinywa wazi maana hata yeye hakutegemea kukuta Kiingereza.
Jambo la pili,ni kwanini isitengenezwe njia rahisi ambayo kila mdau angeweza kujiunga na wadau wengine wa Kiswahili,kama vile njia ya makundi ya mitandao kama whatsapp japo huu huchukua watu wachache sana,basi telegram ambao kundi huweza kuchukua idadi kubwa sana ya watu. Ni maoni tu kuona kama inafaa.
Filipo Lubua
Habari gani Kimaro?
Tunashukuru kuwa umepata fursa ya kutembelea ukurasa wetu. Hata hivyo tumeshindwa kuelewa ni kwanini wewe, pamoja na rafiki yako wa Italia mlishindwa kuona kuwa tovuti yetu ina kurasa pacha, za Kiswahili na Kiingereza. Tafadhali nenda kwenye menyu yetu ya Kiswahili na ufurahie urari wa taarifa zetu katika lugha hiyo.