Leonard Muaka, PhD
Rais wa Chaukidu
Chuo Kukuu cha Howard
Bpepe: muaka@chaukidu.org
Ndugu msomaji, mpenzi wa Kiswahili, mgeni, mkereketwa, na mdau unayeitembelea tovuti hii kwa mara ya kwanza au kwa mara nyingine, tunakukaribisha kwa moyo mkunjufu.
Tuna furaha kuwa umetembelea tovuti ya Chama cha Ukuzaji wa Kiswahili Duniani (CHAUKIDU), chama ambacho ni mali ya mtu yeyote yule anayejitanabaisha kama mzawa, mzungumzaji, mdau, au mrithi wa lugha ya Kiswahili na utamaduni wake. Kwa lugha nyingine, chama hiki kinawaunganisha walimu na wanafunzi wa Kiswahili, watafiti, wanaisimu, waandishi wa kazi bunizi za Kiswahili na wasomaji wao, wasanii, wafanyabiashara, watoa huduma za utalii, wanadayaspora wenye asili ya Afrika Mashariki, na wengine wote ambao wanaipa lugha ya Kiswahili na utamaduni wake nafasi fulani katika maisha yao kwa ujumla.
Kwa mantiki hiyo, hakuna aliyeachwa au ambaye atasema chama hiki si chama chake. Kuanzia mdogo hadi mkubwa, nyote mnakaribishwa kuungana nasi katika harakati na mikakati hii ya kuwaunganisha wadau wote wa Kiswahili. Kama walivyosema wahenga wetu 'umoja ni nguvu, na utengano ni udhaifu', au kama walivyosema pia 'kidole kimoja hakivunji chawa', basi tunakualikeni nyote muungane nasi. Tafadhali pitia tovuti yetu hii ili ujue kwa undani namna chama hiki kiendeshwavyo na jinsi uwezavyo kushiriki. Unakaribishwa sana, na tafadhali mualike mdau mwingine ajiunge nasi. Karibuni nyote wa karibu na wa mbali tuitukuze lugha ya Kiswahili!
Dkt. Filipo Lubua
Mkurugenzi wa Chaukidu
Chuo Kikuu cha Pittsburgh
chaukidu@gmail.com
Please submit your membership payment using the Paypal submit button below
Annual Membership - CHAUKIDU |
Please make a donation using the Paypal submit button below
