Hoteli
Habari ifuatayo ni ya hoteli za DC (group rates) eneo la Silver Spring na pia sehemu iliyoko jirani na Chuo Kikuu cha Howard:
- Days Inn, 8040 13th Street, Silver Spring, MD 20910 (301-588 4400) – $71.20 plus tax
- Holiday Inn Express, 7990 Georgia Avenue, Silver Spring, MD 20910 (301-565 3444) – $115.00 plus tax
- Hampton Inn, 8728 Colesville Road, Silver Spring, MD 2910 (301-588 5887) – $169.00 plus tax
- Double Tree by Hilton, 8727 Colesville Raod Silver Spring, MD 20910 (301-589 5200) – $179.00 plus tax
- Courtyard Marriot, 8506 Fenton Street, Silver Spring Md 20910 (301 589 4899) – $179.00 plus tax
- Courtyard Marriot Washington DC/Capitol Hill, 1325 2nd Street NE Washington DC (202-898 4000) – $179.00 plus tax
Namba 1- 5 ziko Downown Silver Spring ambapo unaweza kupanda Metro Train – Red Line kwenda kokote mjini na pia mabasi (Kuna mabasi yanapitia Georgia Avenue kwenda Howard University). Kwa wale ambao wataenda kwenye Tamasha la usiku sehemu hii itakuwa rahisi kuwafikisha. Namba 6 iko karibu na Chuo Kikuu cha Howard (umbali wa maili 2.6) na iko kwenye Metro Train Red Line, kituo cha Noma/Gallaudet/New York Avenue. Hizo bei zitategemea kama utalipia hoteli mapema. Ukichelewa zinaweza kubadilika!
Usafiri
Kwa usafiri wa ndege mnaweza kuingia DC kwa kupitia uwanja wa National Ronald Reagan (Metro Train – Yellow Line), ambao uko karibu na Downtown Washington DC. Kwa wale ambao watafikia Hilton Hotel Dulles (ALTA Conference site), ni vyema wakapitia uwanja wa Dulles (kuna Shuttle Bus kutoka Airport linakupeleka Metro Train – Wiehle-Reston East station – Silver Line). Kwa wale wanaotaka kukaa Silver Spring, wanaweza pia kupitia uwanja wa BWI- T. Marshall (Amtrack – Silver Spring / Metro Bus – Metro train – Orange Line).
Kama unatoka Uwanja wa Ndege wa Dulles na kuja moja kwa moja kwenye mkutano Howard University, basi itabidi uchukuwe Shuttle Bus Dulles Airport (Washington Flyier) kwenda Kituo cha Metro cha Wiehle-Reston East Station (Silver Line) ambayo itakuleta Washington DC, itabidi kubadilisha treni kwenye kituo cha L’Enfant Plaza na kuingia kwenye Green or Yellow line ambazo zitakupeleka hadi Shaw Howard University Metro Station. Teremka na tembea kama block mbili hivi kuelekea kaskazini kwenye mtaa wa Georgia hadi Howard University. Kwa wale wanaofikia Hilton Hotel, itabidi kuuliza utawala wa Hotel kama kuna Shuttle au njia ya kuwapeleka kwenye kituo cha Metro cha Wiehle-Reston East Station (Silver Line) au uwanjani Dulles Airport ambapo unaweza kuingia kwenye Shuttle Bus. Nauli andaa kama $ 10.00 hivi one way, kwenye shuttle bus ni $ 5.00 na kiasi kama hicho kwenye treni. Ifuatayo ni ratiba ya Shuttle Bus:
Dulles International Airport Silver Line Express Service Schedule
Ticket Prices (each way): Regular Fare: $5.00 per person Airport Employees: $4.00 per person