Usafiri
Uwanja wa ndege wa karibu: Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Entebbe
Usafiri kutoka uwanja wa ndege wa Entebbe hadi Kampala mjini kwa airport tax ni
UGX 100,000/- (laki moja).
Kutoka Kampala mjini hadi Chuo Kikuu cha Kyambogo ni UGX 2,000/- (elfu mbili). Kuna vituo viwili vya daladala (Old park na new park) vya kupandia daladala Kampala.
Unaweza pia kutumia Uber, Bolt, au Safe Boader.
Ikiwa unataka kufanyiwa maandalizi ya mapokezi, kutakuwa na mtu wa kukutoa uwanja wa ndege hadi hotelini kwa gharama nafuu ya UGX 120000/- (laki moja na elfu ishirini). Kupata taarifa hizo, wasiliana na Mwl. Aidah Mutenyo kwa anuani-pepe aidahmutenyo@gmail.com au Mwl. Yunusu Lubuuka kwa anuani-pepe lubuukayunusu@gmail.com.
Taarifa za Hoteli
Kamati ya Maandalizi ya kongamano inapendekeza hoteli zifuatazo kwa ajili ya huduma za malazi kwa washiriki wa kongamano.
Taarifa-za-Hoteli-Kongamano-la-Chaukidu-Uganda