Unaweza kutuma ikisiri yako sasa. Mwisho wa kutuma ikisiri ni Jumapili, Februari 28, 2021. Kutuma ikisiri yako, tafadhali tumia fomu ndogo hapo chini. Ikiwa hujatengeneza wasifu/akaunti katika tovuti ya CHAUKIDU, utahitajika kufanya hivyo ndipo uweze kutuma ikisiri yako. Haitakuchukua zaidi ya dakika mbili kufanya hivyo. Ikiwa ulishajisajili katika tovuti ya CHAUKIDU, utahitaji tu kuingia kwa kutumia jina na nywila ulizotumia wakati unaunda wasifu wako.
Ikisiri zitakazotumwa nje ya utaratibu huu hazitapokelewa na hazitafanyiwa tathmini. Ikiwa unapata tatizo la kiteknolojia, tafadhali wasiliana na watehama wa Chaukidu ama wasiliana na kamati-andalizi na watakupatia msaada unaouhitaji.
Tafadhali ingia hapa ili uweze kutuma au kutathmini ikisiri/mswada
Ingia Ndani
Umesahau Nywila? Weka Upya