CHAUKIDU secretariat@chaukidu.org

Wasiliana Nasi

Mitandao ya Jamii

Kampala 2019

Kongamano la Kimataifa la 5 la Chaukidu

Disemba 13 - 15, 2019 Kampala, Uganda

Chaukidu kingependa kutangaza kongamano la tano la kimataifa na la nne katika eneo la Afrika Mashariki litakalofanyika katika Chuo Kikuu cha Kyambogo, Kampala Uganda. Kongamano hili linaletwa kwenu na Chaukidu kwa kushirikiana na Idara ya Kiswahili ya Chuo Kikuu cha Kyambogo. Mada kuu ni “Ukuaji wa Kiswahili Duniani na Ustawi wa Lugha Nyingine za Kiafrika”. Kongamano hili linalenga kuwaleta pamoja wadau, wazungumzaji, watumiaji na wanataaluma wa Kiswahili kwa ujumla kutoka katika nchi za Afrika Mashariki na Afrika nzima, Marekani, Ulaya na dunia kwa ujumla. 

MahaliChuo Kikuu cha Kyambogo
TareheDisemba 14  - 15, 2019 (Jumamosi na Jumapili)
WarshaIjumaa Disemba 13, 2019
IkisiriJulai 15, 2019
MajibuJuly 30, 2019
Miswada Septemba 30, 2019

 

Tafadhali wasilisha ikisiri yako katika muda uliopangwa. Kupata maelezo zaidi kuhusu kongamano hili, chagua katika menyu iliyoko upande wa kushoto wa ukurasa huu.

Ikiwa ungependa kuchangia kongamano hili, basi unakaribishwa kufanya hivyo. Tuna idadi kubwa ya wanafunzi wa uzamivu na uzamili ambao wangependa kuhudhuria kongamano hili ila wanashindwa kwa sababu ya gharama kubwa. Mchango wako utasaidia kuwafadhili wanafunzi hawa, hasa kwa malazi. Kwa kuchangia, tafadhali tumia kitufe kilichopo hapo chini.

Toa Mchango Wako Hapa