21 - 22 Mei 2021 Mtandaoni
Chaukidu kingependa kutangaza kongamano la mtandaoni (Kongadao) litakalofanyika mwezi Mei 2021 mtandaoni. Mada kuu ni “Hali ya Kiswahili Ulimwenguni: Sasa na Baadaye”. Kongamano hili linalenga kuwaleta pamoja wadau, wazungumzaji, watumiaji na wanataaluma wa Kiswahili kwa ujumla kutoka katika nchi za Afrika Mashariki na Afrika nzima, Marekani, Ulaya, na dunia kwa ujumla.
Mahali | Mtandaoni |
Ikisiri | Februari 28, 2021 |
Majibu | Machi 29, 2021 |
Kuthibitisha | Aprili 26 |
Miswada Makala | Aprili. 30, 2021 (Makala kuchapishwa katika Jarida la CHAUKIDU) |
Tafadhali wasilisha ikisiri yako katika muda uliopangwa. Kupata maelezo zaidi kuhusu kongamano hili, chagua katika menyu iliyoko upande wa kushoto wa ukurasa huu.
Ikiwa ungependa kuchangia kongamano hili, basi unakaribishwa kufanya hivyo. Tuna idadi kubwa ya wanafunzi wa uzamivu na uzamili ambao wangependa kushiriki kongamano hili ila wanashindwa kwa sababu ya gharama mbalimbali. Mchango wako utasaidia kuwafadhili wanafunzi hawa, hasa kwa viingilio na gharama za intaneti. Kwa kuchangia, tafadhali tumia kitufe kilichopo hapo chini.
Toa Mchango Wako Hapa