Mada/Majopo ya Kongamano la Nairobi
- Ukuaji na ukuzaji wa Kiswahili kuwa taaluma ya kiakademia yenye kina na mbinu zake za utafiti (kama taaluma nyinginezo za kisayansi, sayansi-jamii na sanaa-jamii)
- Ufundishaji wa Kiswahili kama lugha ya kigeni
- Ufundishaji wa Kiswahili nyumbani (elimu ya msingi, sekondari, na katika vyuo)
- Kiswahili na/katika vyombo vya habari
- Kiswahili na mitandao ya kijamii (blogu, Facebook, twitter, WhatsApp, n.k.)
- Fasihi ya Kiswahili (riwaya, tamthlia, ushairi)
- Kiswahili na muziki (wa dansi, Taarabu, kizazi kipya, n.k.)
- Kiswahili na sanaa za maigizo (michezo ya redioni, runingani, filamu, n.k.)
- Vibonzo vya Kiswahili
- Kiswahili na ukuaji au udororaji wa demokrasia
- Nafasi ya Kiswahili katika kukuza uchumi wa Afrika Mashariki
- Nafasi ya Kiswahili katika kuimarisha au kudhoofisha jumuiya ya Afrika ya Mashariki
- Nafasi ya Kiswahili katika kupanua ajira kwa vijana
- Utafiti na machapisho ya Kiswahili katika tanzu zake mbalimbali – isimu, lugha, fasihi, n.k.
- Mchango wa Kiswahili katika kukuza au kuua lugha za jamii ndogondogo
- Mchango wa Kiswahili katika kukuza au kuathiri Kiingereza
- Kiswahili na huduma za kijamii
- Leksikolojia na leksikografia ya Kiswahili
- Ufasiri na ukalimani
- Katiba na sheria
- Kiswahili mitaani (matumizi halisi) na chuoni (utafiti, ufundishaji, n.k.)
- Mwanafunzi wa Kiswahili: ufundishaji wa darasani ughaibuni na programu za uzamivu nyumbani
- Usanifishaji na uhurishaji
- Lahaja zinazoibukia: KiSheng, KiSwanglish, n.k.
- Hali ya Kiswahili nchini Rwanda, Burundi, DRC na Uganda
- Kusambaa kwa Kiswahili nje ya bara la Afrika
- Ushirikiano wa wataalamu wa Afrika Mashariki na wa ughaibuni katika utayarishaji wa matini za kufundishia Kiswahili kama lugha ya kigeni
- Nafasi ya teknolojia katika ufundishaji wa Kiswahili
- Mbinu na mikakati mipya/ibuka za kufundisha na kujifunza Kiswahili
- Utamaduni wa Waswahili/Kiswahili
- Tathmini na utahini wa Kiswahili katika madarasa ya Kiswahili kama lugha ya kigeni na kama lugha ya pili (nyumbani)
- Mitihani ya kutathmini uwezo wa wanafunzi wa lugha ya Kiswahili kama lugha ya kigeni