CHAUKIDU secretariat@chaukidu.org

Wasiliana Nasi

Mitandao ya Jamii

Makala Kongandao 2021

Makala zitakazokidhi vigezo vya uchapishaji zitachapishwa katika toleo maalumu la Jarida la Chaukidu. Mwongozo wa makala ni huu ufuatao:

  1. Mswada uwe wa makala au utafiti uliowasilishwa katika Kongamano la Mtandaoni (Kongandao) la Mei 2021. Miswada ya makala ambazo hazikuwasilishwa kwenye kongamano hilo hazitachapishwa katika toleo hili maalumu.
  2. Mswada uandikwe kwa kufuata mwongozo wa APA toleo la 7. Vichwa, aya, marejeleo, na mengine yote katika mswada yazingatie mwongozo wa APA toleo la 7
  3. Mswada uwasilishwe kielektroniki katika mfumo wa Microsoft Word na uzingatie vigezo vifuatavyo:
    1. uwe na maneno kati ya 5000 na 7500 (bila kujumuisha kurasa za marejeleo)
    2. uwe katika hati ya Times New Roman na ukubwa wa maandishi uwe 12 pt
    3. mistari iachane kwa nafasi mbili (double space(
    4. Michoto na picha ziambatishwe pembeni na ziwe katika mfumo wa TIFF au JPG. Ni wajibu wa mwandishi kupata ruhusa ya kutumia michoro au picha zenye hatimiliki.
  4. Mswada uwe na ukurasa wa kwanza ambao utakuwa na kichwa cha wasilisho
  5. Mwandishi asiweke jina lake au jina la chuo chake popote katika mswada
  6. Kuwe na ikisiri ya maneno yasiyozidi 150
  7. Marejeleo yote yaandikwe katika mfumo wa APA toleo la 7
  8. Hakikisha vigezo vyote hivi vimezingatiwa. Mswada ambao hautazingatia maelekezo haya, hautachapishwa wala kufanyiwa tathmini.

Kutuma mswada wako, tumia akaunti yako kuingia katika mfumo wetu wa kielektroniki ambapo utaona mahala pa kutumia makala. Ikiwa huna akaunti katika mfumo wetu, unaweza kuunda akaunti yako hapa pia.