MS-TCDC, Arusha, Tanzania
Kutana na wataalamu, wakereketwa, na wadau wa Kiswahili toka sehemu mbalimbali Duniani. Utafurahi kutangamana na Waswahili wengine na kuwa sehemu ya familia kubwa ya wasemaji wa Kiswahili Duniani! Mada kuu ni "Mnasaba wa Kiswahili na Nyuga Nyingine: Dira ya Mustakabali." Jioni ya tarehe 16 Disemba kutakuwa na tamasha kubwa la Utamaduni wa Mswahili ambapo watu wote wanakaribishwa, hata wale ambao hawakushiriki katika kongamano.