CHAUKIDU secretariat@chaukidu.org

Wasiliana Nasi

Mitandao ya Jamii

Maonyesho

Je, ungependa kuonyesha biashara, kutangaza kazi zako na/au kudhamini kongamano la Chaukidu la mwaka 2015? Kongamano hili litawahusisha na kuwaleta pamoja wakufunzi wa Kiswahili, watafiti, wanafunzi, wanahabari, wasanii, wanaharakati, wanafasihi, wachapishaji, wahudumu wa utalii, taasisi mbalimbali, wakereketwa na wadau wa Kiswahili toka sehemu mbalimbali duniani. Kwa mara ya kwanza kabisa tangu kuanzishwa kwa Chaukidu, kongamano litawaleta wazungumzaji wazawa wa Kiswahili ambao wanaishi katika miji ya Washington, DC, Maryland na Virginia, almaarufu DMV. Kongamano pia litawahudhurisha mabalozi na wanadiplomasia mbalimbali walioko nchini Marekani wakiziwakilisha nchi za Afrika Mashariki na Kati pamoja na jumuiya mbalimbali za Kiafrika.
 
Unaweza kupata moja kati ya vibanda vichache vya maonyesho na matangazo kwa kudhamini kongamano letu na kuwafikia watu wote hawa kutoka Marekani na maeneo mengine duniani. Jina lako na nembo ya biashara yako vitawekwa katika juzuu la ratiba yetu na utaorodheshwa kama miongoni mwa wadhamini wetu wakuu. Vyote hivi utavipata kwa ada ndogo ya $100 tu! Kama ungependa kunyakua nafasi moja kati ya hizi, tafadhali lipia nafasi hiyo kwa kubofya kitufe kilichoko hapo chini.