CHAUKIDU secretariat@chaukidu.org

Wasiliana Nasi

Mitandao ya Jamii

Uchaguzi 2019

Tangazo Maalumu Na. 008: Matokeo ya Uchaguzi wa Chaukidu 2019

Kwa wanachama wote wa CHAUKIDU,

Kamati ya Katiba na Uchaguzi (KKU) inayo furaha kuwajulisha kwamba mchakato wa uchaguzi wa viongozi wapya wa CHAUKIDU umemalizika vyema na tayari KKU imemaliza kufanya zoezi la kupitia na kuhakiki matokeo. Tunawashukuruni nyote mlioshiriki kufanikisha zoezi hili. Yafuatayo ni matokeo rasmi ya uchaguzi huo. Soma Zaidi

Tangazo Maalumu Na. 007: Kuongezwa Muda

Tume ya Katiba na Uchaguzi (KKU) inatangaza kwamba imeongeza muda wa kupiga kura kwa siku mbili za jumamosi na jumapili. Sababu kubwa ambayo imezingatiwa katika uamuzi huu ni ukweli kwamba muda uliokuwa umewekwa kuanzia jumatatu hadi Ijumaa ni muda wa kazi na huenda baadhi ya wanachama hawakuweza kupata nafasi ya kwenda kwenye sehemu zenye intaneti (Internet Cafe) kutimiza wajibu na haki yao ya kupiga kura. KKU inatambua kwamba siyo kila mtu ana simu ya mkononi yenye uwezo wa kuwa na mtandao wakati wote (internet). Soma Zaidi

Tangazo maalumu Na. 006: Shahada za Kupigia Kura

Kwa wanachama wote wa CHAUKIDU

Hivi punde mtaanza kupokea karatasi au shahada za kupigia kura kutoka kwa BallotBin na ujumbe ufuatao:..... Soma Zaidi

Tangazo Muhimu Na. 005

Kwa wanachama wote wa CHAUKIDU,

Wakati tunajiandaa kukamilisha zoezi la upigaji kura na kuwapata viongozi wapya, Kamati ya Katiba na Uchaguzi (KKU) ingependa kutoa ufafanuzi ufuatao.

Kwanza tunaomba kuwahakikishia wanachama wote wa CHAUKIDU kwamba KKU inatekeleza wajibu wake kwa weledi wa hali ya juu ikizingatia katiba ya chama, kanuni za uchaguzi na haki za kila mwanachama. Kwa mujibu wa Katiba ya CHAUKIDU, kila mwanachama anayo haki ya kugombea nafasi yoyote ya uongozi iwe moja, mbili, tatu au zaidi. Wanachama wote walipewa nafasi hiyo. Wajibu wa mpiga kura ni kupima kila mgombea kwa nafasi zote alizoomba na kuamua kumpigia mgombea huyo kura yako kwa nafasi moja, mbili, tatu au zaidi alizoomba...... Soma Zaidi

Tangazo Muhimu Na. 004: Wagombea

Kwa Wanachama Wote wa CHAUKIDU,
Kwanza tunafurahi kuwajulisha kwamba zoezi la kupokea mapendekezo ya wagombea wa uongozi wa chama limekwenda vizuri. Mwitikio ulikuwa mzuri sana na majina ya wanachama zaidi ya 30 yalipendekezwa kuwania nafasi mbali mbali za uongozi. Baada ya kuwasiliana na waliopendekezwa kuuliza uafiki wao, baadhi yao walitoa udhuru kwa sababu mbali mbali. Kamati ya Katiba na Uchaguzi inachukua fursa hii kutangaza rasmi majina ya wanachama waliokubali kugombea nafasi za uongozi wa chama.... Soma Zaidi

Tangazo Muhimu Na. 003: Kuongezwa Muda

Kufuatia maamuzi ya kikao cha Bodi ya CHAUKIDU kilichofanyika tarehe 10 Machi 2019, Kamati ya Katiba na Uchaguzi (KKU) inatangaza rasmi kwamba muda wa kupokea mapendekezo ya wagombea umeongezwa na tarehe ya mwisho ya kupokea mapendekezo ya wagombea ni jumatano Machi 20, 2019.

Uchaguzi huu utahusisha viongozi wafuatao: Rais, Makamu wa Rais, Mkurugenzi, Naibu Mkurugenzi, Mweka Hazina na Katibu Mwenezi wa Chama pia wajumbe sita wa Bodi wa kuchaguliwa. Kulingana na Katiba nafasi zingine kwenye Bodi zitajazwa na wajumbe wa kuteuliwa na Bodi mpya ya uongozi.

Tuma mapendekezo yako haraka kabla ya muda uliotajwa hapo juu kwisha. Tunaomba utume mapendekezo yako moja kwa moja kwenye anuani ifuatayo ya Kamati ya Katiba na Uchaguzi ya CHAUKIDU: <kkuchaukidu@gmail.com>. Soma Zaidi

Tangazo Muhimu # 002: Kupendekeza Majina

Kwa mujibu wa Katiba ya Chama, vifungu namba 5.5, 6.3, 6.4 na 6.4.1, Kamati ya Katiba na Uchaguzi (TKU) ingependa kuwajulisha kwamba mchakato wa uchaguzi wa viongozi wa juu wa Chama na wajumbe wa Bodi umeanza rasmi. Uchaguzi huu utahusisha viongozi wafutao: Rais, Makamu wa Rais, Mkurugenzi, Naibu Mkurugenzi, Mweka Hazina na Katibu Mwenezi wa Chama pia wajumbe wengine sita ambao kwa pamoja wataunda Bodi ya Uongozi. Soma Zaidi

Tangazo Muhimu Na. 001: Kusasisha Kumbukumbu

Kwa wanachama na wakereketwa wote wa CHAUKIDU,

Kamati teule ya Katiba na Uchaguzi ingependa kuwajulisha kwamba kama ilivyoazimiwa katika mkutano mkuu wa mwaka uliopita, tutakuwa na uchaguzi wa viongozi wa CHAUKIDU mwaka huu. Kamati imeanza maandalizi ya mchakato wa uchaguzi ambao unalenga kukamilisha zoezi la uchaguzi ifikapo kati kati ya mwezi Aprili mwaka huu. Soma Zaidi