CHAUKIDU secretariat@chaukidu.org

Wasiliana Nasi

Mitandao ya Jamii

Usafiri Kilifi 2021

Basi

Kuna mabasi kutoka Tanzania hadi mombasa. Unaweza kuingi Mombasa kupitia Arusha-Moshi-Voi. Unaweza pia kupitia Tanga kisha Mombasa. Aidha unaweza kupitia Nairobi kwa wale waliokaribu na Nairobi. Kwa walioko Uganda, wapitie Nairobi. Kwa walioko Burundi na Rwanda wapitie Tanzania, kisha Nairobi na badae Mombasa/Malindi. Mabasi yapo kutoka Nairobi hadi Malindi au Mombasa. Chuo Kikuu cha Pwani kiko kando tu ya barabara.

Kuna kampuni za mabasi zifuatazo: Dreamline, Modern Coast, Tahmeed, Chania Genesis, Bus Car, na Mash

  1. Nairobi hadi Kilifi, daraja la kwanza ni Ksh 2500
  2. Nairobi hadi Kilifi, kawaida ni Ksh 1600 hadi 1800
  3. Nairobi hadi Mombasa, daraja la kwanza ni Ksh 2000
  4. Nairobi hadi Mombasa, kawaida 1200 hadi 1600
Treni

Kuna treni kutoka Nairobi hadi Mombasa, kituo cha kushukia kiko karibu na uwanja wa ndege Mombasa. Kuna mabasi au matatu kutoka hapo hadi Mombasa mjini. Aidha, unaweza kupanda matatu za Mtwapa na kutoka hapo utachukua matatu za kilifi. Kamati ya maandalizi inaongea na uongozi wa chuo kuomba basi la chuo lichukue washiriki wa kongamano toka kituo cha treni

  1. Nairobi hadi Mombasa, daraja la kwanza ni Ksh 3000
  2. Nairobi hadi Mombasa, kawaida 1200 hadi 1000
Ndege

Kuna wiwanja viwili vya ndege ambavyo washiriki wa kongamano wanaweza kutumia - uwanja wa ndege wa Kimataifa Malindi na ule wa Kimataifa Mombasa (Moi). Ni vyema kutumia awanja wa Malindi sababu upo karibu zaidi na chuo cha Pwani kuliko wa Mombasa; pia hauna msongamano mkubwa wa magari