Usajili katika Kongamano
Ili kuhudhuria kongamano la CHAUKIDU Disemba 2016, ni muhimu ujisajili. Tunawahimiza wote wafikirie kujisajili kama wanachama wa CHAUKIDU. Unaweza kujisajili mtandaoni kupitia ukurasa wa CHAUKIDU ambao una kiungo cha PayPal. Ikiwa hili haliwezekani, usajili unaweza kufanywa wakati wa kongamano bila faini.
Viwango vya Ada
Hadhira | Usajili wa Awali | Usajili wa Kawaida |
Wanafunzi wote(Tumia kitambulisho cha chuo) | Ksh. 1000.00 au $10.00 | Ksh. 1000.00 au $10.00 |
Washiriki wengine wa Afrika Mashariki na barani kote. | Ksh. 2000.00 au $20.00 | Ksh. 2000.00 au $20.00 |
Washiriki wengine wote kutoka nje ya Afrika | Ksh. 15000 au $150.00 | Ksh. 15000 au $150.00 |
Kiingilio |
Gharama ya Dhifa (tarehe 16/12/2016)
Dhifa itakayofanywa siku ya Ijumaa jioni itahusisha chakula cha Kiafrika, divai, vinywaji visivyo vya pombe na burudani (hai). Tutahitaji kujua mapema kidogo wale watakaopenda kushiriki. Itakuwa fahari ya kamati andalizi ikiwa wageni wote watashiriki. Gharama ya dhifa ni kama ifuatavyo:
Hadhira | Malipo |
Washiriki wote | Ksh. 1500.00 au $15.00 |
Uanachama wa CHAUKIDU
Ili kulipia uanachama wa CHAUKIDU, tafadhali utembelee ukurasa wa CHAUKIDU (chaukidu.org). Tungependa kuwahimiza nyote kujiunga na Chama rasmi. Bofya Hapa Kujiunga na Chama.