Usajili na Ada ya Kongamano
Ili kuhudhuria kongamano la CHAUKIDU Disemba 2019 jijini Kampala, Uganda, ni muhimu sana ujisajili. Tunawahimiza wote mfikirie kujisajili kama wanachama wa CHAUKIDU kwanza kabla ya kujisajili kwa ajili ya kongamano. Unaweza kujisajili mtandaoni kupitia ukurasa wa CHAUKIDU ambao una kiungo cha PayPal. Pia unaweza kujisajili na kulipia ada yako kwa njia za simu. Utaratibu utaletwa kupitia njia mbalimbali za mawasiliano, ikiwemo WhatsApp na barua pepe. Ikiwa haiwezekani kufanya usajili kwa kutumia njia hizo, usajili unaweza kufanywa pia wakati wa kongamano bila faini.
Warsha
Kutakuwa na warsha zitakayotolewa siku moja kabla ya kongamano, tarehe 13 Disemba kwa gharama ndogo ya $10 na $5 kwa wanafunzi. Warsha hizi zitalenga maeneo mawili muhimu sana katika ufundishaji wa Kiswahili kama lugha ya kigeni: Warsha ya kwanza itakuwa katika ujumuishaji wa U5 (au 5Cs, kama ziitwavyo kwa Kiingereza). Warsha hii itatolewa na wataalamu wabobezi katika ufundishaji wa Kiswahili kama lugha ya kigeni Prof. Kiarie Wa'Njogu kutoka chuo Kikuu cha Yale, na Dkt. Beatrice Ng'uono kutoka Chuo Kikuu cha Baylor. Warsha ya pili itakuwa katika matumizi ya teknolojia za kidijitali katika ufunzaji wa Kiswahili kama lugha ya kigeni. Warsha hii itasimamiwa na Dkt. Filipo Lubua kutoka Chuo Kikuu cha Pittsburgh pamoja na daktari tarajali Mwl. Malimi Kazi kutoka Chuo KIkuu cha Duquesne.
Warsha hizi zitatolewa ikiwa tu watakuwepo watu wenye hitaji hilo. Kila warsha itachukua wakurufunzi wasiozidi 40, kwa hiyo wale watakaowahi kujiandikisha ndiyo watakaopata nafasi. Kujiandikisha, utapaswa kujaza fomu ya usajili. Katika fomu hiyo unaombwa kueleza ikiwa una uzoefu wowote wa kufundishaji Kiswahili kama lugha ya kigeni na kuorodhesha vipengele vya ufundhishaji ambavyo ungependa wakufunzi wa warsha wavigusie. Kujaza fomu ya warsha, tafadhali bofya hapa.
Viwango vya Ada
Hadhira | Gharama za Usajili |
Wanafunzi (Tumia kitambulisho cha chuo) | $20 |
Washiriki kutoka Afrika Mashariki | $40 |
Washiriki kutoka Barani Afrika | $50 |
Washiriki kutoka nje ya Afrika | $150 |
Lipia Usajili Hapa
Uanachama wa CHAUKIDU
Ili kulipia uanachama wa CHAUKIDU, tafadhali utembelee ukurasa wa CHAUKIDU (chaukidu.org). Tungependa kuwahimiza nyote kujiunga na Chama rasmi. Bofya Hapa Kujiunga na Chama.