CHAUKIDU secretariat@chaukidu.org

Wasiliana Nasi

Mitandao ya Jamii

Usajili na Ada ya Kongandao 2021

Ili kushiriki kongamano la CHAUKIDU Mei 2021 mtandaoni, Kenya, ni muhimu sana ujisajili. Tunawahimiza wote mfikirie kujisajili kama wanachama wa CHAUKIDU kwanza kabla ya kujisajili kwa ajili ya kongamano, na hilo litakusaidia kulipa ada ya kongamano ya wanachama ambayo, ina punguzo. Unaweza kujisajili mtandaoni kupitia ukurasa wa CHAUKIDU ambao utakuwezesha kufanya malipo yako kwa PayPal ama kwa kadi yako ya benki. Pia unaweza kujisajili na kulipia ada yako kwa njia ya simu kwa kuwasiliana na wawakilishi waliotajwa.

Pia, ukilipa ada yako mapema utapata punguzo. Ada za usajili wa kongamano kwa makundi mbalimbali zimeainishwa katika jedwali hapo chini. 

Viwango vya Ada ya Kongandao

Kujisajili

Ikiwa wewe ni mwanachama aliyelipia ada ya mwaka huu, fungua kiungo hiki ili ulipie ada ya kongamano. Ikiwa wewe si mwanachama uliyelipia ada ya mwaka huu, fungua kiungo hiki kulipia ada yako ya kongamano. Kumbuka unaweza kulipa ada ya uanachama kwanza na kisha ulipe ada ya kongamano kama mwanachama. Hiyo itakusaidia kulipia kongamano kwa kiwango cha wanachama ambacho kiko chini zaidi. 

Kulipia Uanachama wa CHAUKIDU

Tungependa kuwahimiza nyote kujiunga na Chama rasmi ili mpate faida nyingi wazipatazo wanachama waliolipia ada. Kujua aina na kulipia uanachama wa CHAUKIDU, tafadhali tembelea ukurasa wa Unachama ambao uko hapa chaukidu.org/uanachama