Mpenzi Mwanachama Tarajali,
Mwaliko wakujiunga
Tunayo furaha kukuletea mwaliko huu wa kujiunga na CHAUKIDU, chama kitakachokuunganisha na wadau mbalimbali wa Ksiwahili duniani. Kama mmoja wa watu wenye (au watarajiao kuwa na) mahusiano na Afrika ya Mashariki, lugha ya Kiswahili na utamaduni wake, tunaamini jumuiya hii itakunufaisha. Vilevile tunaamini kuwa utaifaidisha pia jumuiya hii kwa mawazo yako na uanachama wako. Kwa hiyo, uanachama wako utakuwa ni hatua muhimu sana ya kutuwezesha kufikia moja ya malengo yetu - kuwapa watu wote duniani fursa ya kujiunga na jumuiya yenye umuhimu mkubwa.
Kama una swali lolote, tafadhali usisite kuwasiliana na Mkurugenzi Mtendaji kupitia mussahans30@gmail.com au Rais wa CHAUKIDU kupitia lubua@pitt.edu.