Mada kuu ni “Mnasaba wa Kiswahili na Nyuga Nyingine: Dira ya Mustakabali.” Jioni ya tarehe 16 Disemba, kutakuwa na tamasha kubwa la Utamaduni wa Mswahili, ambapo watu wote wanakaribishwa, hata wale ambao hawakushiriki katika kongamano.
Kongamano la Kimataifa la CHAUKIDU linakuwa fursa ya kujumuika katika harakati za kukuza na kueneza lugha ya Kiswahili
Kongamano hili litakupa fursa ya kusikiliza mawasilisho ya mada elekezi kutoka kwa wasemaji mahiri na waliobobea katika fani zao.
Kongamano hili linakupa fursa ya kukutana na watu mbalimbali toka sehemu mbalimbali za dunia. Kutana na watu wapya kongamanoni!
Ili kulifurahia kongamano, utahitaji mahali pazuri pa malazi. Kamati-andalizi imewaandalia malazi ndani ya chuo cha MS TCDC na nje karibu na chuo. Japo chaguo ni lako, hakikisha unahifadhi malazi mapema ili upate mahala ambapo utapafurahia zaidi.
Profesa Mstaafu wa Isimu Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Tanzania
Profesa wa Isimu ya Afrika Chuo Kikuu cha Masomo ya Kigeni cha Hankuk Korea Kusini
Katika makongamano yote ya CHAUKIDU, ikisiri hutumwa kwa mfumo maalumu wa ikisiri. Mfumo huu huwezesha upokeaji na utathmini wa ikisiri zote. Bofya hapa kutuma ikisiri yako.
Naweza kutuma ikisiri yangu wapi?
Unakuwa mwanachama hai wa CHAUKIDU kwa kulipa ada ya kila mwaka. Lipa ada yako uwe mwanachama hai sasa.
Ni jinsi gani ya kuwa mwanachama hai wa CHAUKIDU?
Hapana. CHAUKIDU si chama cha walimu pekee. Ni chama cha wadau na wakereketwa wote wa Kiswahili.
CHAUKIDU ni chama cha Walimu tu?
© Tutorim 2024. All rights reserved