CHAUKIDU secretariat@chaukidu.org

Wasiliana nasi

+1 (740) 591-8749

Kuhusu Kongamano Hili​

Kuhusu Kongamano Hili​

Kutana na wataalamu, wakereketwa, na wadau wa Kiswahili toka sehemu mbalimbali Duniani. Utafurahi kutangamana na Waswahili wengine na kuwa sehemu ya familia kubwa ya wasemaji wa Kiswahili Duniani! Mada kuu ni “Mnasaba wa Kiswahili na Nyuga Nyingine: Dira ya Mustakabali.” Jioni ya tarehe 16 Disemba, kutakuwa na tamasha kubwa la Utamaduni wa Mswahili, ambapo watu wote wanakaribishwa, hata wale ambao hawakushiriki katika kongamano.
Kamati ya maandalizi inaangalia uwezekano wa kuandaa shughuli za kitalii zitakazofanyika siku ya Jumapili, Disemba 17. Wale watakaohitaji kushiriki katika utalii watajulishwa gharama zitakuwa kiasi gani na ni maeneo gani ya kiutalii yatakayotembelewa.

0%

Kongamano la Kimataifa la CHAUKIDU linakuwa fursa ya kujumuika katika harakati za kukuza na kueneza lugha ya Kiswahili​

Kongamano hili litakupa fursa ya kusikiliza mawasilisho ya mada elekezi kutoka kwa wasemaji mahiri na waliobobea katika fani zao. ​

Kongamano hili linakupa fursa ya kukutana na watu mbalimbali toka sehemu mbalimbali za dunia. Kutana na watu wapya kongamanoni!​

Je, umeshajiwekea malazi?

Hoteli na Malazi

Je, umeshajiwekea malazi?

Hoteli na Malazi

Ili kulifurahia kongamano, utahitaji mahali pazuri pa malazi. Kamati-andalizi imewaandalia malazi ndani ya chuo cha MS TCDC na nje karibu na chuo. Japo chaguo ni lako, hakikisha unahifadhi malazi mapema ili upate mahala ambapo utapafurahia zaidi.

Haya ni malazi ya viwango mbalimbali yapatikanayo ndani ya chuo. Kamati-Andalizi imefanya mazungumzo na idara ya malazi chuoni na kupewa bei za punguzo kwa wakongamanaji. Jihifadhie malazi mapema ili kukwepa usumbufu unaoweza kujitokeza.

Haya ni malazi ya viwango mbalimbali yapatikanayo nje ya chuo. Kamati-Andalizi imefanya mazungumzo na idara ya malazi chuoni na kupewa bei za punguzo kwa wakongamanaji. Jiwekee malazi mapema ili kukwepa usumbufu unaoweza kujitokeza.

Wasemaji Wetu

Nani ni Wasemaji Wakuu?

Prof. F.E.M.K. Senkoro - Makala Elekezi

Profesa Mstaafu wa Isimu Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Tanzania

Prof. Jina Jina - Makala Maalumu

Profesa wa Isimu ya Afrika Chuo Kikuu cha Masomo ya Kigeni cha Hankuk Korea Kusini
Kwanini Hutakiwi Kukosa?

Usikose Kongamano Lenye Hadhi ya Kidunia

Hili ni kongamano lenye hadhi ya kidunia. Litawaleta wadau kutoka nchi na maeneo mbalimbali duniani. Kuwa sehemu ya familia kubwa ya Waswahili kote ulimwenguni. Usikose!

Address

2816 Cathedral of Learning, Pittsburgh, PA 15260

Phone

+1 (740) 591-8749

email

makongamano@chaukidu.org

Wasiliana Nasi

Wasiliana Nasi

Wasiliana nasi kupitia hii form au mitandao ya jamii

Mayasa

Maswali Yaulizwayo Sana

Kuna maswali ambayo wadau wetu wanayauliza mara kwa mara. Tafadhali angalia kama swali ulilokuwa nalo limejibiwa humu:

Faham zaidi...
Naweza kutuma ikisiri yangu wapi?

Katika makongamano yote ya CHAUKIDU, ikisiri hutumwa kwa mfumo maalumu wa ikisiri. Mfumo huu huwezesha upokeaji na utathmini wa ikisiri zote. Bofya hapa kutuma ikisiri yako.

Ni jinsi gani ya kuwa mwanachama hai wa CHAUKIDU?

Unakuwa mwanachama hai wa CHAUKIDU kwa kulipa ada ya kila mwaka. Lipa ada yako uwe mwanachama hai sasa.

Je CHAUKIDU ni chama cha Walimu tu?

Hapana. CHAUKIDU si chama cha walimu pekee. Ni chama cha wadau na wakereketwa wote wa Kiswahili.