Kongamano la Kimataifa la 6 la Chaukidu
Disemba 15 - 18, 2021 Kilifi, Kenya
Chaukidu kingependa kutangaza kongamano la sita la kimataifa na la tano katika eneo la Afrika Mashariki litakalofanyika katika Chuo Kikuu cha Pwani, Kilifi Kenya. Kongamano hili linaletwa kwenu na Chaukidu kwa kushirikiana na Idara ya Kiswahili ya Chuo Kikuu cha Pwani. Mada kuu ni “Kiswahili na Viswahili: Kuelekea Karne Moja ya Usanifishaji”. Kongamano hili linalenga kuwaleta pamoja wadau, wazungumzaji, watumiaji na wanataaluma wa Kiswahili kwa ujumla kutoka katika nchi za Afrika Mashariki na Afrika nzima, Marekani, Ulaya na dunia kwa ujumla.
Mahali | Chuo Kikuu cha Pwani |
Warsha | Disemba 15, 2021 (Jumatano) |
Kongamano | Disemba 16 - 17, 2021 (Alhamisi na Ijumaa) |
Utalii | Jumamosi, Disemba 18, 2021 |
Ikisiri | Mei 30, 2021 |
Majibu | Julai 15, 2021 |
Kuthibitisha | Septemba 30, 2021 |
Miswada Makala | Dis. 31, 2021 (Makala kuchapishwa katika Jarida la CHAUKIDU) |
Tafadhali wasilisha ikisiri yako katika muda uliopangwa. Kupata maelezo zaidi kuhusu kongamano hili, chagua katika menyu iliyoko upande wa kushoto wa ukurasa huu.
Ikiwa ungependa kuchangia kongamano hili, basi unakaribishwa kufanya hivyo. Tuna idadi kubwa ya wanafunzi wa uzamivu na uzamili ambao wangependa kuhudhuria kongamano hili ila wanashindwa kwa sababu ya gharama kubwa. Mchango wako utasaidia kuwafadhili wanafunzi hawa, hasa kwa malazi. Kwa kuchangia, tafadhali tumia kitufe kilichopo hapo chini.
Toa Mchango Wako Hapa