CHAUKIDU secretariat@chaukidu.org

Usajili Kilifi 2021

Usajili na Ada ya Kongamano

Ili kuhudhuria kongamano la CHAUKIDU Disemba 2021 mjini Kilifi, Kenya, ni muhimu sana ujisajili. Tunawahimiza wote mfikirie kujisajili kama wanachama wa CHAUKIDU kwanza kabla ya kujisajili kwa ajili ya kongamano. Unaweza kujisajili mtandaoni kupitia ukurasa wa CHAUKIDU ambao una kiungo cha PayPal. Pia unaweza kujisajili na kulipia ada yako kwa njia ya simu. Utaratibu utaletwa kupitia njia mbalimbali za mawasiliano, ikiwemo WhatsApp na barua pepe. Ada za usajili kwa makundi mbalimbali zimeainishwa katika jedwali hapo chini.

Warsha

Kutakuwa na warsha zitakayotolewa siku moja kabla ya kongamano, tarehe 15 Disemba kwa gharama ndogo ya $10 na $5 kwa wanafunzi. Mada zitakazotolewa kwenye warsha zitaletwa kwenu pale utaratibu utakapokamilika. 

Kujisajili

Ikiwa wewe ni mwanachama aliyelipia ada ya mwaka huu, fungua kiungo hiki ili ulipie ada ya kongamano. Ikiwa wewe si mwanachama uliyelipia ada ya mwaka huu, fungua kiungo hiki kulipia ada yako ya kongamano. Kumbuka unaweza kulipa ada ya uanachama kwanza na kisha ulipe ada ya kongamano kama mwanachama. Hiyo itakusaidia kulipia kongamano kwa kiwango cha wanachama ambacho kiko chini zaidi. 

Kulipia Uanachama wa CHAUKIDU

Tungependa kuwahimiza nyote kujiunga na Chama rasmi ili mpate faida nyingi wazipatazo wanachama waliolipia ada. Kujua aina na kulipia uanachama wa CHAUKIDU, tafadhali tembelea ukurasa wa Unachama ambao uko hapa chaukidu.org/uanachama