CHAUKIDU secretariat@chaukidu.org

Wasiliana Nasi

Mitandao ya Jamii

Kilifi 2021

Kongamano la Kimataifa la 6 la Chaukidu

Disemba 15 - 18, 2021 Kilifi, Kenya

Chaukidu kingependa kutangaza kongamano la sita la kimataifa na la tano katika eneo la Afrika Mashariki litakalofanyika katika Chuo Kikuu cha Pwani, Kilifi Kenya. Kongamano hili linaletwa kwenu na Chaukidu kwa kushirikiana na Idara ya Kiswahili ya Chuo Kikuu cha Pwani. Mada kuu ni Kiswahili na Viswahili: Kuelekea Karne Moja ya Usanifishaji”. Kongamano hili linalenga kuwaleta pamoja wadau, wazungumzaji, watumiaji na wanataaluma wa Kiswahili kwa ujumla kutoka katika nchi za Afrika Mashariki na Afrika nzima, Marekani, Ulaya na dunia kwa ujumla. 

Mahali Chuo Kikuu cha Pwani
Warsha Disemba 15, 2021 (Jumatano)
Kongamano Disemba 16  - 17, 2021 (Alhamisi na Ijumaa)
Utalii Jumamosi, Disemba 18, 2021
Ikisiri Mei 30, 2021
Majibu Julai 15, 2021
Kuthibitisha  Septemba 30, 2021
Miswada Makala
Dis. 31, 2021 (Makala kuchapishwa katika Jarida la CHAUKIDU)

 

Tafadhali wasilisha ikisiri yako katika muda uliopangwa. Kupata maelezo zaidi kuhusu kongamano hili, chagua katika menyu iliyoko upande wa kushoto wa ukurasa huu.

Ikiwa ungependa kuchangia kongamano hili, basi unakaribishwa kufanya hivyo. Tuna idadi kubwa ya wanafunzi wa uzamivu na uzamili ambao wangependa kuhudhuria kongamano hili ila wanashindwa kwa sababu ya gharama kubwa. Mchango wako utasaidia kuwafadhili wanafunzi hawa, hasa kwa malazi. Kwa kuchangia, tafadhali tumia kitufe kilichopo hapo chini.

Toa Mchango Wako Hapa