UCHAGUZI WA CHAUKIDU 2019
TAARIFA ZA WAGOMBEA WA NAFASI ZA UONGOZI
RAIS |
Dk. Dainess Maganda ni mkurugenzi wa kitengo cha lugha, tamaduni na fasihi za Kiafrika katika chuo kikuu cha Georgia. Nimekuwa mwalimu wa Kiswahili kwa zaidi ya miaka kumi. Nimekitumikia chama hiki katika nyanja mbalimbali miaka iliyopita, kama mwana bodi na mweka hazina. Ninajivunia lugha yangu ya Kiswahili. Naamini kwamba lugha ya Kiswahili ni ya muhimu sana na nimechukua jukumu la kuitangaza lugha hii na utamaduni wake kwa kutumia fasihi, utafiti, kupeleka wanafunzi Tanzania na pia nimeanzisha miradi ya ufundishaji wa Kiswahili kwa wazee na watoto kama huduma katika jamii mbalimbali zilizoko katika mji ninaoishi. Nimefanikiwa kutunukiwa tuzo kadhaa za ufundishaji ikiwepo na tuzo ya ufundishaji bora katika chuo hiki mwaka jana (2018). Naamini kwamba sisi sote tuliopewa zawadi hii ya kujua lugha ya Kiswahili tuna jukumu la kujivunia lugha yetu na kuwafanya wengine waipende na kuithamini. Ingawa nilizaliwa Tanzania, kwa sasa ninaishi na familia yangu katika mji wa Athens, jimbo la Georgia, Marekani.
Dk. Leonard Muaka ni profesa mshrikishi katika Chuo Kikuu cha Howard, Washington DC, Marekani, ambako pia ni mratibu wa lugha za Kiafrika. Utaalamu wake ambao unadhihirika katika utafiti, uchapishaji na ufundishaji, umejikita zaidi katika maswala ya kiisimu kama vile pragmatiki, isimujamii, mofolojia, uchanganuzi wa kiisimu wa usemi, ufundishaji wa lugha za kigeni, upokeaji(upataji) wa lugha ya pili, na fashi ya Afrika. Prof. Muaka ana tajriba kubwa ya kufundisha Kiswahili, Kiingereza, isimu, na fasihi katika vyuo vikuu mbalimbali nchini Kenya, Marekani na Mexico. Huduma zake katika taaluma za kiakademia ni nyingi. Kwa sasa anamalizia awamu yake ya urais wa Chama cha Walimu wa Lugha za Kiafrika (ALTA). Aidha, amekihudumia chama cha CHAUKIDU kikamilifu kama mkurugenzi mtendaji na kusaidia kukikuza chama hadi sasa. Pia yeye ni mwanabodi katika Shirikisho la Kitaifa la Vyama vya Walimu wa Lugha za Kisasa yaaniNational Federation of Modern Language Teachers Associations (NFMLTA) ambako hushughulikia maswala ya fedha na ufadhili wa utafiti. Falsafa inayouelekeza uongozi wake na utoaji wa huduma ya hali ya juu ni “kwa kujituma”. Lengo lake kubwa barani Afrika na ughaibuni ni kuzijenga lugha za Kiafrika na kuzipa hadhi nje na ndani ya bara la Afrika kwa kuwashirikisha wadau wote. Kwa awamu hii, ambayo itakuwa ya mwisho kwake, lengo kuu ni kuendeleza huduma nzuri za bodi ya sasa na kukiimarisha chama kifedha, kuvihusisha vyuo Marekani, Asia, Uropa, na Afrika kuwa wanachama, kuwahamasisha wadau wote nje ya akademia, kuzingatia msingi dhabiti na maadili ya CHAUKIDU, na kuimarisha miradi ya kuwafaa wasomi na vijana wanaoibuka kiakademia. Kwake, yote yanawezekana iwapo kila mmoja ana nia na maono ya kukijenga chama kivifae vizazi vijavyo bila kujifikiria kwanza. Imani yake ya kimsingi ni, Ukiona vinaelea ujue vimeundwa!
MAKAMU WA RAIS |
Dk. Dainess Maganda ni mkurugenzi wa kitengo cha lugha, tamaduni na fasihi za Kiafrika katika chuo kikuu cha Georgia. Nimekuwa mwalimu wa Kiswahili kwa zaidi ya miaka kumi. Nimekitumikia chama hiki katika nyanja mbalimbali miaka iliyopita, kama mwana bodi na mweka hazina. Ninajivunia lugha yangu ya Kiswahili. Naamini kwamba lugha ya Kiswahili ni ya muhimu sana na nimechukua jukumu la kuitangaza lugha hii na utamaduni wake kwa kutumia fasihi, utafiti, kupeleka wanafunzi Tanzania na pia nimeanzisha miradi ya ufundishaji wa Kiswahili kwa wazee na watoto kama huduma katika jamii mbalimbali zilizoko katika mji ninaoishi. Nimefanikiwa kutunukiwa tuzo kadhaa za ufundishaji ikiwepo na tuzo ya ufundishaji bora katika chuo hiki mwaka jana (2018). Naamini kwamba sisi sote tuliopewa zawadi hii ya kujua lugha ya Kiswahili tuna jukumu la kujivunia lugha yetu na kuwafanya wengine waipende na kuithamini. Ingawa nilizaliwa Tanzania, kwa sasa ninaishi na familia yangu katika mji wa Athens, jimbo la Georgia, Marekani.
Dk. Hadija Jilala: Nina elimu ya PhD ( Kiswahili), Master of Arts (Linguistics),Bachelor of Education (Arts) Majoring in Kiswahili, shahada zote hizo nimesomea Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Tanzania. Nimeajiliwa na Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, Kitivo cha Sanaa na Sayansi za Jamii, Idara ya Isimu na Taaluma za Fasihi tangu Disemba 2006. Kituo changu cha kazi ni makao makuu ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania yaliyopo Kinondoni jijini Dar es salaam. Cheo changu cha kitaaluma ni Mhadhiri Mwandamizi wa Kiswahili nimebobea katika tafsiri na isimu. Aidha, nimefundisha katika vyuo mbalimbali kama mwalimu wa muda. Mpaka sasa nimefanya tafiti za kitaaluma na kuchapisha makala 13, vitabu viwili na nimehariri kitabu kimoja. Mpaka sasa nina makala 14 nilizowasilisha katika makongamano ya kitaifa na kimataifa na bado hazichapishwa na zingine zipo katika hatua ya kuchapishwa na majarida mbalimbali. Vilevile nina miswada ya vitabu 6 ambayo haijachapishwa na ipo katika mkakati wa kuchapishwa.
Ninafundisha kozi za Kiswahili katika ngazi mbalimbali kuanzia Kiswahili kwa wageni, shahada ya kwanza, umahiri na uzamivu, ninafanya tafiti na miradi ya lugha, utamaduni, isimu na fasihi ya Kiswahili. Vile vile ninasimamia tafiti za isimu na fasihi ya Kiswahili katika ngazi za umahiri na uzamivu. Aidha, ninatoa ushauri wa kitaalamu (hususan tafsiri na uhariri) katika taasisi za serikali na zisizo za serikali na pia katika mashirika ya kimataifa. Mpaka sasa nimetafsiri nyaraka za vitabu vya Kiingereza kwenda lugha ya Kiswahili vipatavyo 7. Nimetafsiri mfumo wa ujifunzaji Kielektroniki (Moodle learning system) kutoka lugha ya Kiingereza kwenda Kiswahili.
Dk. Musa Hans anafundisha Kiswahili Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Ana Shahada ya Uzamivu (Kiswahili), shahada ya Uzamili (Lugha) na Shahada ya Elimu (Arts); alipata shahada zote hizi toka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Tanzania. Dr. Musa Hans Ameandika makala na vitabu mbali mbali vy Kiswahili; pia amehuduria makongamano mengi ya yahusuyo lugha ya Kiswahili.
MKURUGENZI |
Dk. Filipo Lubua ni mhadhiri katika idara ya isimu ya Chuo Kikuu cha Pittsburgh kilichopo jimbo la Pennsylvania, nchini Marekani. Ni mhitimu wa shahada ya Sanaa na Elimu (B.A. Ed.) katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Ni mhitimu pia wa shahada ya uzamili katika Isimu Tumizi (M.A. Applied Ling.) katika Chuo Kikuu cha Ohio, nchini Marekani, ambapo alitaalamikia eneo la ujifunzaji wa lugha kwa lutumia teknolojia ya kompyuta (Computer-Assisted Language Learning). Baada ya kuhitimu shahada ya uzamili, alijiunga na masomo ya uzamivu katika Teknolojia ya Ufundishaji (Instructional Technology) katika chuo hicho hicho. Tasnifu yake ya uzamivu iliangazia maswala ya ujasiriamali-taaluma katika teknolojia ya ufundishaji, hasahasa ufundishaji wa lugha kwa kutumia teknolojia ya kompyuta.Dk. Lubua ni mpenzi wa Kiswahili na teknolojia. Pia ni mshairi, mwimbaji, na mwandishi wa riwaya. Hadi sasa amechapisha mashairi lukuki na riwaya iitwayo Kilele Kiitwacho Uhuru iliyochapwa na Jomo Kenyatta Foundation (2014). Amewasilisha na kufanya machapisho mbalimbali yanayoangazia maswala ya matumizi ya teknolojia katika ufundishaji na ujifunzaji wa lugha. Katika CHAUKIDU, Dk. Lubua amekuwa Mjumbe wa Bodi tangu mwaka 2014 na amekuwa akitumika katika ofisi ya teknolojia, hasahasa uundaji na uhariri wa tovuti ya Chaukidu. Pia ameshiriki katika kamati mbalimbali zikiwemo kamati za maandalizi ya makongamano, kamati za katiba na uchaguzi, kamati ya tuzo, na kamati ya uhamasishaji na ufadhili. Katika kipindi chote alichokuwa mjumbe wa bodi na wa kamati mbalimbali, Dk. Lubuaamejifunza mambo mengi yakiwemo uwajibikaji na ushirikiano katika kutekeleza majukumu.
NAIBU MKURUGENZI |
Dk. David W. Kyeu ni Mhadhiri wa lugha ya Kiswahili na Mratibu wa walimu wa lugha za kiafrika. Alipokea shahada ya uzamifu katika lugha za kiafrika kutoka chuo kikuu cha Wisconsin Madison. Utafiti wake ulichunguza jinsi wanafunzi wa Kiswahili kama lugha ya kigeni waliweza kuandika insha baada ya kuwa na mawasiliano ya ana kwa ana, na kwenye komputa. Mwalimu Kyeu alipokea mafunzo ya PhD minor kwenye ujifunzaji lugha ya pili (SLA), na anayo shahada ya uzamili katika Kiswahili na taaluma zake kutoka chuo kikuu cha Egerton. Shahada yake ya kwanza ilikuwa ya elimu katika isibati na Kiswahili. Dkt. Kyeu anayo tajriba ya zaidi ya miaka 10 ya kufundisha nchini Marekani, Uswidi na Kenya. Hivi sasa, Dkt. Kyeu ni msimamizi wa programu ya lugha za kiafrika katika chuo kikuu cha California, Berkeley. Vilevile ni mhadhiri katika idara ya wamarekani wa asili ya kiafrika.
MWEKA HAZINA |
Mwl. Happiness Patrick: Mhadhiri wa Kiswahili katika Chuo Kikuu cha Cornell kilichopo Ithaca New York, Marekani. Anasomea shahada ya Uzamivu katika uwanda wa elimu ya kimataifa, ufundishaji, na uboreshaji wa mitaala. Chuo Kikuu cha North Central, Marekani. Ana elimu ya shahada ya Uzamili katika Isimu na Ufundishaji wa Lugha. Chuo Kikuu cha Oregon, Marekani. Ana elimu ya shahada ya Awali katika Sanaa na Elimu, Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam, Tanzania.
Sasa anafundisha Kiswahili katika Chuo kikuu cha Cornell. Kabla ya kuja Cornell, alifundisha Kiswahili chuo Kikuu cha Oregon tangu mwaka 2009. Kwa sasa pia ni mshauri wa masuala ya lugha ya Kiswahili kwenye; ufundishaji, utathmini wa maendeleo ya ustadi wa kuzungumza lugha ya Kiswahili kwa ufasaha kama lugha ya kigeni na utengenezaji mitaala, nyenzo za kufundishia, na teknolojia. Amethibitishwa na Baraza la Kiamerika la Ufundishaji Lugha za Kigeni (ACTFL OPI ILR Swahili Langauge Tester) kupima na kutathmini viwango vya ustadi wa uzungumzaji kwa wazungumza Kiswahili kama lugha ya kigeni. Pamoja na kuwa mwanachama wa CHAUKIDU, Happinesss ni mwanachama wa Chama cha Waalimu wa Lugha za Kiafrika (ALTA) na Baraza la Kiamerika la Ufundishaji wa Lugha za Kigeni (ACTFL).
KATIBU MWENEZI |
Beatrice Mkenda ni Mwalimu wa Kiswahili katika chuo kikuu Cha Iowa. Amekuwa katibu wa Chaukidu kwa takriban miaka mitatu. Licha ya kufundisha Kiswahili na utamaduni, Mwalimu Mkenda amekuwa akiegemeza utafiti wake kwenye masuala ya ufundishaji wa lugha za kigeni katika nyanja za matini ya kufundisha, teknolojia, fasihi, na utamaduni.
WAJUMBE WA BODI |
Mwl. Aida Mutenyo ni Mhadhiri wa isimu na fasihi katika Kiswahili. Taaluma yangu ni isimu na fasihi katika Kiswahili though napenda sana 2nd language teaching and acquisition.
Nafundisha chuo KIkuu cha Kyambogo kwa sasa ila mwezi ujao nitajiunga na chuo KIkuu Kabale.
Prof. Aldin K. Mutembei ni Mhadhiri wa lugha ya Kiswahili na Mtembei ni Mgoda, Kigoda cha Uprofesa cha Mwalimu Nyerere katika Kiswahili. Na amewahi kuwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Ukuzaji wa Kiswahili ya Chuo Kikuu cha Dar es Saalam. Prof. Aldin Mtembei ana Shahada ya Uzamivu toka Chuo Kikuu cha Leuden, Netherland ambapo alitalamikia maswala ya mashairi. Pia ana Shahada ya Uzamili toka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambapo alijikita katika maswala ya fonolojia katika mashairi ya Kiswahili. Aidha Prof. Mtembei ana Shahada ya Sanaa na Elimu katika masomo ya Kiswahili na History.
Mwl. Esther Martin Simba ni mwalimu wa Kiswahili kwa wageni wanaotaka kujifunza Kiswahil kama lugha ya pili. Nina digrii ya pili kutoka chuo kikuu cha Dar es Salamu, 2014. Nina makazi Moshi, Kilimanjaro na Arusha; ninaishi sehemu zote kutokana na shughuli. Nimewahi kufundisha shule za msingi, shule za sekondari na vyuo vya ualimu. Nilifanya pia kazi na US Peace Corps Tanzania kwa miaka 12 kama mwalimu wa Kiswahili na utamaduni na baadae kufikia ngazi ya mratibu wa mafunzo hayo na kisha kuwa mkurugenzi msaidizi wa mafunzo ya US Peace Corps Tanzania. Katika kipindi hicho niliwahi pia kuwa mtahini wa lugha (Language Tester) kwa muda mrefu. Kwa sasa mimi ni mkurugenzi mtendaji wa kampuni yangu inayoitwa Experience Tanzania Co. Ltd. yenye miaka 11 sasa. Kampuni inajihusisha na utalii, kufundisha Kiswahili kwa wageni, utamaduni, kuendesha programu za wanafunzi kutoka duniani kote pamoja na watu wazima kwa kushirikiana na wabia mbalimbali, malazi, chakula, kuwajengea uwezo vijana na wanawake, n.k.
Dk. Hadija Jilala: Nina elimu ya PhD ( Kiswahili), Master of Arts (Linguistics),Bachelor of Education (Arts) Majoring in Kiswahili, shahada zote hizo nimesomea Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Tanzania. Nimeajiliwa na Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, Kitivo cha Sanaa na Sayansi za Jamii, Idara ya Isimu na Taaluma za Fasihi tangu Disemba 2006. Kituo changu cha kazi ni makao makuu ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania yaliyopo Kinondoni jijini Dar es salaam. Cheo changu cha kitaaluma ni Mhadhiri Mwandamizi wa Kiswahili nimebobea katika tafsiri na isimu. Aidha, nimefundisha katika vyuo mbalimbali kama mwalimu wa muda. Mpaka sasa nimefanya tafiti za kitaaluma na kuchapisha makala 13, vitabu viwili na nimehariri kitabu kimoja. Mpaka sasa nina makala 14 nilizowasilisha katika makongamano ya kitaifa na kimataifa na bado hazichapishwa na zingine zipo katika hatua ya kuchapishwa na majarida mbalimbali. Vilevile nina miswada ya vitabu 6 ambayo haijachapishwa na ipo katika mkakati wa kuchapishwa.
Ninafundisha kozi za Kiswahili katika ngazi mbalimbali kuanzia Kiswahili kwa wageni, shahada ya kwanza, umahiri na uzamivu, ninafanya tafiti na miradi ya lugha, utamaduni, isimu na fasihi ya Kiswahili. Vile vile ninasimamia tafiti za isimu na fasihi ya Kiswahili katika ngazi za umahiri na uzamivu. Aidha, ninatoa ushauri wa kitaalamu (hususan tafsiri na uhariri) katika taasisi za serikali na zisizo za serikali na pia katika mashirika ya kimataifa. Mpaka sasa nimetafsiri nyaraka za vitabu vya Kiingereza kwenda lugha ya Kiswahili vipatavyo 7. Nimetafsiri mfumo wa ujifunzaji Kielektroniki (Moodle learning system) kutoka lugha ya Kiingereza kwenda Kiswahili.
Dk. Musa Hans anafundisha Kiswahili Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Ana Shahada ya Uzamivu (Kiswahili), shahada ya Uzamili (Lugha) na Shahada ya Elimu (Arts); alipata shahada zote hizi toka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Tanzania. Dr. Musa Hans Ameandika makala na vitabu mbali mbali vy Kiswahili; pia amehuduria makongamano mengi ya yahusuyo lugha ya Kiswahili.
Mwl. Mwajuma Selemani Mohamedi (Madam Nice). Naishi Tanga Tanzania. Ni Muajiriwa katika Halmashauri ya jiji la Tanga na pia ni kiongozi wa CHALUFAKITA kanda ya Kaskazini. Katika ngazi za uongozi nilizowahi kupitia ni pamoja na kuwa Muweka hazina na Makamu Mwenyekiti wa CHAWAKAMA Chuo Kikuu cha Dodoma(COED) na Mwenyekiti wa muda wa Kanda ya Kaskazini katika utafiti uliofanywa na (KAKAMA). Tuzo nilizowahi kupata ni pamoja na tuzo ya Mwalimu mbunifu wa kiswahili kutoka CHALUFAKITA mwaka 2017. Pamoja na Mshindi wa hadithi fupi shindalo lililoendeshwa na CULTURE LINK AFRICA LTD. 2019. Vile vile mimi ni mtunzi wa Riwaya tamthilia, hadithi fupi pamoja na filamu. Na kwa sasa kitabu changu kilichokamilika kinajulikana kwa jina la "NDOA YA USALITI". Naombeni mnichague kuwa MJUMBE WA BODI YA CHAUKIDU
Prof. Pacifique Malonga works at African Academy of Languages, Kiswahili Commissioner, Coordinator of BECOS Rwanda, Kigali, Rwanda. He is a Coordinator of BECOS , (an independent languages promotion office) in Kigali, a writer, researcher and trainer of Kiswahili with Radio and TV programs
Dk.Pendo Malangwa ni Mwalimu wa Kiswahili Chuo Kikuu Dar es Salaam, Tanzania
Mwl. Yusta Mganga ni Mwalimu wa Kiswahili MSTCD, Arusha Tanzania
Dk. Zeinab Idd ni Mwalimu wa Kiswahili Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar