CHAUKIDU secretariat@chaukidu.org

Blog Details

Shahada za Kura

Kwa wanachama wote wa CHAUKIDU Hivi punde mtaanza kupokea karatasi au shahada za kupigia kura kutoka kwa BallotBin na ujumbe ufuatao:

Uchaguzi wa Viongozi wa Chaukidu 2019

This is a message from Uchaguzi Chaukidu from Chaukidu, who is using Ballotbin.com to run the survey/election: Ndugu mwanachama wa Chaukidu, Kamati ya Katiba na Uchaguzi (KKU) inakushukuru kwa ushirikiano uliouonyesha tangu mwanzo wa mchakato huu wa uchaguzi wa Bodi mpya ya chama chetu. Tumefikia hatua ya mwisho kabisa ya mchakato huu, na hapa tunakutumia shahada yako ya kupigia kura. Piga kura yako kwa kufuata maelekezo uliyopewa kutoka katika tovuti ya BallotBin. Uchaguzi utaanza tarehe 1 Aprili 2019 saa sita kamili usiku (12:00AM) na utafungwa tarehe 5 Aprili saa tano na dakika hamsini na tisa usiku (11:59 PM). Hutoweza kupiga kura kabla na baada ya muda uliotajwa hapo juu, kwa hiyo tunakuomba uzingatie muda huo. Utapiga kura yako kwa kuchagua Rais, Makamu wa Rais, na Wajumbe Sita wa Bodi ya Chaukidu. Ikiwa kuna mahala panakukanganya kidogo, basi wasiliana na KKU kupitia anuani-pepe yao: kkuchaukidu@gmail.com. Tutajitahidi kujibu ujumbe wako haraka itakavyowezekana. Asante sana, Dk. Elias Magembe Kny: KKU                                                             CLICK HERE TO VOTE
Huu ni ujumbe halali kwa hiyo tunaomba usiufute. Endapo hutauona kwenye sanduki lako la Inbox, angalia kwenye kapu la Junk au Spam. Utapiga kura moja tu, hata kama utapokea barua-pepe mbili au zaidi, mfumo huu utaruhusu kupokea kura moja tu kutoka kwenye shahada ulopewa kupitia anuani-pepe yako. Kwa ufafanuzi wa muda, saa zilizotajwa ni saa za Marekani, upande wa pwani ya mashariki (Eastern Time Zone), kwa maana hiyo wapigaji wa Afrika Mashariki wanaweza kuanza kupiga kura saa moja asubuhi jumatatu tarehe 1 April na kuendelea hadi saa kumi na mbili na dakika hamsini na tisa asubuhi jumamosi tarehe 6 April. Wanachama walioko katika maeneo mengine ya dunia mtalinganisha muda wenu kulingana na maelezo haya.  Asanteni sana. Dk. Elias J. Magembe Kny. Kamati ya Katiba na Uchaguzi (KKU) – CHAUKIDU
Releted Tags
    Share:

    Leave a comment