CHAUKIDU secretariat@chaukidu.org

Blog Details

#ChaukiduKilifi2021: Muda wa Ikisiri Umeongezwa

Tuma Ikisiri yako Sasa! Kongamano la Kimataifa la Kilifi 2021
WanaChaukidu na Wadau wa Kiswahili popote mlipo, kongamano la CHAUKIDU la mwaka 2021litafanyika katika Chuo Kikuu cha Pwani, Kilifi Kenya, tarehe 15 – 17 Disemba 2021. Kongamano hilo litakuwa ni mwendelezo wa makongamano ya kimataifa ya Chaukidu ambayo yalianza mwaka 2015 mjini Washington, DC, na yakaendelea katika miji na nchi mbalimbali: Nairobi, Kenya (2016), Dar es Salaama, Tanzania (2017), Zanzibar, Tanzania (2018), na Kampala, Uganda (2019). Wale waliokwisha kuhudhuria makongamano haya watashuhudia jinsi yalivyo makongamano ya aina yake, yakiwaleta watu kutoka mahala mbalimbali duniani. Mwaka huu huko Kilifi, kongamano litakuwa bora sana, pengine kuliko makongamano yote ambayo Chaukidu imewahi kuyafanya. Tunakishukuru sana Chuo Kikuu cha Pwani kwa kukubali kudhamini kongamano hili mwaka huu wa 2021 tena.
Kamati-andalizi inayoongozwa na Dkt. Kiarie Wa’Njogu iliongeza muda wa kutuma ikisiri mpya ama kufanyia masahihisho ikisiri zilizotumwa mwaka jana. Tarehe ya mwishi ya kufanya hivyo ni Jumamosi, tarehe 10 Julai, 2021. Tafadhali zingatieni yafuatayo:
  1. Wale ambao hawakutuma ikisiri mwaka jana, wamepewa nafasi nyingine ya kutuma ikisiri zao mwaka huu. Mwisho ni Jumamosi tarehe 10 Julai.
  2. Wale waliokwisha kutuma ikisiri na zikafanyiwa tathmini na kukubalika, ikisiri zo ziko salama na zitatumika ikiwa wanahitaji kuzitumia hizohizo. Watatumiwa barua rasmi za mwaliko.
  3. Kama ulituma ikisiri mwaka jana ikakubalika lakini ungetaka kuwasilisha ikisiri nyingine tofauti na ile uliyokuwa umeituma, unaruhusiwa kutuma ikisiri nyingine. Ila unapaswa kuijulisha kamati-andalizi kuwa ungependa kuiondoa ikisiri yako ya awali.
  4. Ikiwa ulituma ikisiri yako mwaka jana na baada ya tathmini ikisiri yako ikakataliwa, unaweza kuifanyia ikisiri yako marekebisho na kuituma tena, au unaweza kutuma ikisiri nyingine mpya kabisa.
Kwa swali lolote lihusianalo na kongamano la Kilifi, tafadhali tuma barua-pepe kwa kupitia anuani ifuatayo: ChaukiduPwani2020@gmail.com. Kwa taarifa zaidi kuhusu ChaukiduKilifi2021, tembelea tovuti yetu ambayo ni: https//kilifi2021.chaukidu.org.
Bofya Hapa Kutuma Ikisiri Yako
Twitter
Facebook
Website
Email
Instagram
ShareShare
TweetTweet
ForwardForward
This email was sent to *|EMAIL|* why did I get this?    unsubscribe from this list    update subscription preferences *|LIST:ADDRESSLINE|* *|REWARDS|*
Releted Tags
    Share:

    Leave a comment