CHAUKIDU secretariat@chaukidu.org

Blog Details

Kupendekeza Majina

Tangazo Muhimu # 002: Kupendekeza Majina

Kwa mujibu wa Katiba ya Chama, vifungu namba 5.5, 6.3, 6.4 na 6.4.1, Kamati ya Katiba na Uchaguzi (TKU) ingependa kuwajulisha kwamba mchakato wa uchaguzi wa viongozi wa juu wa Chama na wajumbe wa Bodi umeanza rasmi. Uchaguzi huu utahusisha viongozi wafutao: Rais, Makamu wa Rais, Mkurugenzi, Naibu Mkurugenzi, Mweka Hazina na Katibu Mwenezi wa Chama pia wajumbe wengine sita ambao kwa pamoja wataunda Bodi ya Uongozi. Hatua ya kwanza ni kupokea mapendekezo (nominations) kutoka kwa wanachama walio hai. Unaweza kujipendekeza au kupendekeza mwanachama mwingine kwa nafasi moja au zaidi ya moja. Endapo unapendekeza jina la mwanachama mwingine ni jukumu lako kuhakikisha kwamba huyo unayempendekeza yuko tayari kushika wadhifa unaopendekezwa. Tunaomba utume mapendekezo yako moja kwa moja kwenye anuani ifuatayo ya Kamati ya Katiba na Uchaguzi ya CHAUKIDU: <kkuchaukidu@gmail.com>. Ili uweze kushiriki kikamilifu katika uchaguzi huu (kuchagua au kuchaguliwa), ni muhimu kuhakikisha kwamba wewe ni mwanachama hai wa CHAUKIDU na uwe umelipa ada yako ya uanachama hadi mwaka huu wa 2019.  Tafadhali usisahau kutupatia anuani yako ya barua pepe ambayo tutaitumia kuwasiliana na wewe moja kwa moja. Tunaomba utume mapendekezo yako haraka sana, kabla ya tarehe 10 mwezi Machi 2019. Changamkia fursa ya kuwapata viongozi mahiri wa chama ambao watatuongoza kwa kipindi kijacho, shiriki kikamilifu katika mchakato wa uchaguzi wa CHAUKIDU – 2019. Asanteni sana Dr. Elias J. Magembe Kny. Kamati ya Katiba na UchaguziCHAUKIDU
Releted Tags
    Share: