UCHAGUZI WA VIONGOZI WA CHAUKIDU 2021 Tangazo la Kuanza Kupokea Mapendekezo ya Wagombea
1.0 UTANGULIZI
1.1. Kama tulivyowatangazia hapo awali, TKU inapenda kuwakaribisha wanachama kugombea nafasi mbalimbali za uongozi wa chama cha CHAUKIDU kwa kipindi cha miaka miwili ifuatayo (April 2021- April 2023).
1.2. Dirisha la kutoa mapendekezo ya wagombea limefunguliwa rasmi na TKU itaanza kupokea mapendekezo hayo kuanzia tarehe 15 hadi 28 Februari 2021. Mapendekezo yanakaribishwa kutoka kwa mwanachama yeyote aliye hai (ambaye amelipa ada yake ya uanachama angalau hadi mwaka huu, 2021).
1.3 Mwanachama hai anaweza kujipendekeza yeye mwenyewe au kumpendekeza mwanachama mwingine, ili mradi ahakikishe huyo anayempendekeza yu mwanachama hai (yaani, amelipa ada yake ya uanachama angalau hadi mwaka huu, 2021) na yuko tayari kutumikia nafasi anayompendekezea. Kwa mujibu wa katiba, maafisa wanaoshikilia nafasi za uongozi kwa kipindi cha sasa pia wanaruhusiwa wagombee tena nafasi hizo au nafasi nyingine za uongozi.
2. NAFASI ZA UONGOZI
TKU inapenda kuwakaribisha wanachama kugombea nafasi zifuatazo za uongozi wa chama cha CHAUKIDU kwa kipindi cha miaka miwili ifuatayo (April 2021/April 2023).
- Rais
- Makamu wa Rais
- Mkurugenzi
- Naibu Mkurugenzi
- Mweka Hazina (Mhazini)
- Katibu Mwenezi wa Chama
- Wajumbe sita (6) wa Bodi ya Wakurugenzi
3.0 UTARATIBU
3.1. Tuma mapendekezo yako moja kwa moja kwa Tume ya Katiba na Uchaguzi (TKU) kwa kutumia anani ya barua pepe ifuatayo: kkuchaukidu@gmail.com
3.2. Mbali na kutuma jina la mgombea na nafasi anayopendekezwa kuwania, TKU pia inaomba kupata sifa za mgombea kwa ufupi, uzoefu wake katika maswala ya uongozi na msukumo au mtazamo wake wa kiuongozi, hususani kwa chama cha CHAUKIDU.
3.3. Jina la mgombea linaweza kupendekezwa kuwania zaidi ya nafasi moja ya uongozi.
4.0 HITIMISHO
4.1. TKU inapenda kuwakumbusha wanachama wote wahakikishe kwamba wako hai (yaani, wawe wamelipa ada zao za uanachama angalau hadi mwaka huu, 2021) ili waweze kuwa na haki ya kumpendekeza mgombea, kugombea nafasi ya uongozi, kupiga kura na kupigiwa kura).
4.2 Endapo una swali lolote au dukuduku lolote, usisite kututumia ujumbe moja kwa moja kwa njia ya barua pepe kwenye anwani ifuatayo: kkuchaukidu@gmail.com
Kumbuka: ili uweze kupiga kura au kupigiwa kura lazima ulipe ada yako