CHAUKIDU secretariat@chaukidu.org

Mulika – Chaukidu Nairobi 2016

Taasisi ya Taaluma za Kiswahili (TATAKI) Chuo Kikuu cha Dar es Salaam

Mulika 2017 Toleo Maalum Makala ya Kongamano la Chaukidu Nairobi 2016

 

MULIKA ni jarida la taaluma ya Lugha na Fasihi ya Kiswahili. Jukumu lake kuu ni kukusanya na kusambaza maarifa yanayohusu Lugha na Fasihi ya Kiswahili yaliyokitwa katika utafiti mpevu. MULIKA limeendelea kuwa daraja kati ya watumiaji wa Kiswahili popote walipo, na wataalamu wa Kiswahili katika shule za Sekondari na Vyuo vya Elimu ya Juu Afrika ya Mashariki. Jarida huchapishwa mara moja kwa mwaka. Jarida linapokea makala yaliyoandikwa kwa Kiswahili TU. Makala yapigwe chapa kwenye karatasi z fasi mbili. Upande mmoja tu wa karatasi utumiwe.

Toleo hili Maalumu la Mulika ni zao la ushirikiano kati ya Taasisi ya Taaluma za Kiswahili (TATAKI) na Chama cha Ukuzaji wa Kiswahili Duniani (CHAUKIDU). Makala ya chapisho hili yametokana na Kongamano la CHAUKIDU lililofanyika Nairobi, Kenya, Desemba 16-17, 2016. Kongamano hilo lilihudhuriwa na wajumbe kutoka nchi mbalimbali duniani, pamoja na Mkurugenzi wa TATAKI, Dkt. Ernesta Mosha. Wakati wa mazungumzo kati ya uongozi wa CHAUKIDU na TATAKI, Taasisi iliombwa, na ikakubali, kushirikiana na CHAUKIDU kuchapisha Toleo Maalumu la makala ya Kongamano hilo. Imetuchukua takriban mwaka mmoja kukusanya na kuhariri makala ya toleo. Tunawashukuru sana waandishi na wasomaji wetu kwa uvumilivu wao. Kupakua na kusoma makala za toleo hili, utapaswa kununua. Unaweza ukanunua jarida zima ($49.99) au makala mojamoja ($9.99). Kununua, unaweza kutembelea duka la CHAUKIDU au kufungua viungo vifuatavyo kulingana na mahitaji yako.

Toleo Maalum la Makala ya Kongamano la CHAUKIDU 2017 Jarida zima

  1. Tahariri (Bure)
  2. Utangulizi (Leonard Muaka, Anne Jebet, David Kyeu na Beatrice Mkenda) (Bure)
  3. Makala Elekezi: Kiswahili na Umajumui wa Kiafrika (M. M. Mulokozi)
  4. Taswira za Hali na Maana katika Nyimbo za Kizazi Kipya: Kundi la Offside Trick (Anne Mwari)
  5. Mchango wa Kihindi Katika Leksikografia ya Kiswahili (Benard Odoyo Okal)
  6. Malumbano ya Mchongoano: Je, Huchongoa au Kudumaza Watoto Kielimu na Kimaadili? (Clara Momanyi)
  7. Mchango wa `Kiriku` Katika Makuzi ya Fasihi ya Watoto (Deborah Nanyama Amukowa)
  8. Nyimbo Shambulizi za Bongo Fleva Katika Siasa Liberali Tanzania (Fokas Nchimbi)
  9. Ubeberu wa Kiisimu na Mustakabali wa Lugha za Kiafrika: Mapitio ya Sera ya Lugha Tanzania (Gervas A. Kawonga)
  10. Majina ya Wahusika katika Fasihi ya Kiswahili (Hilda Pembe)
  11. Maadili ya Kisiasa Katika Riwaya za Kiswahili: Kufa Kuzikana na Babu Alipofufuka (Justus Kyalo Muusya na Kitula King’ei)
  12. Kiswahili na Ukombozi wa Jamii (Kiarie Wa’njogu)
  13. Kiswahili Marekani (Lioba Moshi) Mitindo ya Lugha Ibuka katika Mitandao ya Kijamii: Mifano Kutoka Mawasiliano ya Facebook (Toboso Mahero Bernard, Mosol Kandagor na Allan Opijah)
  14. Athari za Mafunzo-Kazini: Mfano Halisi wa Walimu wa Kiswahili Katika Shule za Upili Garissa (Geoffrey Nyaega Mogere, & Moses Wasike)
  15. Dhima ya Ujozi Lugha katika Kufanikisha Mawasiliano: Mifano Kutoka Sajili ya Mchezo wa Kandanda (Mark A. Odawo) Fasihi katika Lahaja Ibukizi. Mifano kutoka Chapisho la “Shujaaz” (Pamela Ngugi)
  16. Nafasi ya Lugha Katika Kukabiliana na Changamoto za Kijamii, Kiuchumi na Kisiasa Afrika (Prisca Jebet Kiprotich) Nafasi ya Kiswahili Katika Mawasiliano ya Kijamii: Uchanganuzi wa Ujumbe Mfupi Unaosambazwa kwa Wagonjwa wa UKIMWI Nchini Kenya (Sarah Ndanu M. Ngesu)
  17. Wahusika, Uhusika na Mtazamo Katika Riwaya ya Kiswahili (Susan Kawira na Simiyu Kisurulia)