CHAUKIDU secretariat@chaukidu.org

Blog Details

Jarida la Mulika: Toleo Maalumu la Makala za Kongamano la Nairobi Disemba 2016

$49.99

Toleo hili Maalumu la Mulika ni zao la ushirikiano kati ya Taasisi ya Taaluma za Kiswahili (TATAKI) na Chama cha Ukuzaji wa Kiswahili Duniani (CHAUKIDU). Makala ya chapisho hili yametokana na Kongamano la CHAUKIDU lililofanyika Nairobi, Kenya, Desemba 16-17, 2016. Kongamano hilo lilihudhuriwa na wajumbe kutoka nchi mbalimbali duniani, pamoja na Mkurugenzi wa TATAKI, Dkt. Ernesta Mosha. Wakati wa mazungumzo kati ya uongozi wa CHAUKIDU na TATAKI, Taasisi iliombwa, na ikakubali, kushirikiana na CHAUKIDU kuchapisha Toleo Maalumu la makala ya Kongamano hilo. Imetuchukua takriban mwaka mmoja kukusanya na kuhariri makala ya toleo. Tunawashukuru sana waandishi na wasomaji wetu kwa uvumilivu wao.

SKU: Nairobi2016Nzima Category:

Description

Hili ni jarida zima kabisa. Utaweza kupakua jarida hili na makala zake zote ukishakamilisha malipo.
Releted Tags
    Share: