CHAUKIDU secretariat@chaukidu.org

Blog Details

Mkutano Mkuu wa Mwaka

Kwa mujibu wa katiba yetu, kila mwaka tunapaswa kuwa na Mkutano Mkuu unaowashirikisha wanachama wote. Mkutano huo tumekuwa tukiufanya katika makongamano ya ALTA/CHAUKIDU ya mwezi wa Aprili, ila kwa sababu mwaka huu kongamano hilo ambalo lilikuwa lifanyikie jijini Chicago, Marekani halikufanyika, viongozi na bodi ya CHAUKIDU wameona ni vyema mkutano huo ufanyike kwa njia ya Zoom. Mkutano huo utafanyika Ijumaa, tarehe 26 Juni 2020, saa 6:00 mchana hadi saa 8:00 mchana (kwa masafa ya EDT) ambayo itakuwa saa 1:00 – 3:00 usiku kwa Tanzania, Kenya, na Uganda (saa 12:00 – 2:00 usiku kwa Burundi na Rwanda). Pamoja na agenda nyingine katika mkutano huo, wanachama wataletewa taarifa mbalimbali za chama, ikiwemo taarifa ya fedha, pamoja na mipango ya chama kwa mwaka 2020/2021. Pia wanachama watapigia kura mabadiliko madogo ya katiba ambayo yataletwa kwenu na Tume ya Katiba na Uchaguzi (TKU) kwa niaba ya Bodi. Watu wote wataruhusiwa kushiriki katika mkutano huo, lakini wale ambao hawajalipa ada ya mwaka huu hawataruhusiwa kupiga kura. Hivyo, tunaanza rasmi usasishaji wa daftari letu utakaoenda sambamba na ulipaji wa ada. Tumeisasisha tovuti yetu ili iwezeshe watu kujisajili na kulipia ada ya uanachama. Wakusanyaji wetu wa kila eneo watakusanya ada pia kwa niaba ya chama. Wanachama hai wote watakaohitaji watapewa cheti cha uanachama kwa mwaka huu. Utaratibu zaidi wa namna ya kujisajili utaletwa kwenu.

Releted Tags
    Share:

    Leave a comment