CHAUKIDU secretariat@chaukidu.org

Blog Details

Mkutano Mkuu wa Mwaka 2021

Kwa mujibu wa katiba yetu, kila mwaka tunapaswa kuwa na Mkutano Mkuu unaowashirikisha wanachama wote. Kamatulivyofanya mwaka jana 2020, Mkutano Mkuu wa mwaka huu utafanyika tena kwa njia ya Zoom. Mkutano huo utafanyika Jumapili, tarehe 16 Mei 2021, saa 4:00 Asubuhi hadi saa 6:00 mchana (kwa masafa ya EST) ambayo itakuwa saa 11:00 – 1:00 Jioni kwa Tanzania, Kenya, na Uganda (saa 10:00 – 12:00 Jioni kwa Burundi, Rwanda, na Kongo). Pamoja na agenda nyingine katika mkutano huo, wanachama wataletewa taarifa mbalimbali za chama, ikiwemo taarifa ya fedha, pamoja na mipango ya chama kwa mwaka 2021/2022. Pia wanachama watashughulikia makabidhiano ya ofisi yatakayofanywa na Bodi ya Mwaka 2019 -2021 kwenda kwa Bodi ya 2021 -2023. Hafla ya makabidhiano itasimamiwa na TUme ya Katiba na Uchaguzi. Watu wote wataruhusiwa kushiriki katika mkutano huo, lakini wale ambao hawajalipa ada ya mwaka huu hawataruhusiwa kupiga kura. Hivyo, tunaanza rasmi usasishaji wa daftari letu utakaoenda sambamba na ulipaji wa ada. Tumeisasisha tovuti yetu ili iwezeshe watu kujisajili na kulipia ada ya uanachama. Wakusanyaji wetu wa kila eneo watakusanya ada pia kwa niaba ya chama. Wanachama hai wote watakaohitaji watapewa cheti cha uanachama kwa mwaka huu. Utaratibu zaidi wa namna ya kujisajili utaletwa kwenu.

Releted Tags
    Share:

    Leave a comment