CHALUFAKITA kilianzishwa mnamo Agosti 14, 2014 na wapenzi wa lugha ya Kiswahili kwa shabaha ya kuwaunganisha pamoja Watanzania wote bila kubagua ili kuilea, kuiongoza, kuikuza, kuihuisha, pamoja na kuipa maana na hadhi Lugha na Fasihi ya Kiswahili. Kilisajiliwa na Msajili wa Vyama vya Kijamii mnamo Februari 2016.
Jarida la CHALUFAKITA
Jarida la Chama cha Lugha na Fasihi ya Kiswahili Tanzania (CHALUFAKITA) linamilikiwa na chama hicho ambacho makao makuu yake ni Dodoma,Tanzania. Jarida la CHALUFAKITA lilianzishwa na kusajiliwa tarehe 18/01/2018. Hili ni jarida la kimataifa linalochapisha makala zake mara moja kwa mwaka. Jarida linapatikana katika nakala ngumu pamoja na nakala tepe/mkondoni. Jarida hili limesajiliwa pia na African Journals Online (AJOL). Lengo la Jarida ni kuendeleza na kudumisha lugha ya Kiswahili na utamaduni wa Waswahili. Pia, linalenga kuwajengea uwezo wanataaluma katika kufanya tafiti na kuandika makala mbalimbali zitakazochangia maarifa mapya katika nyuga mbalimbali za lugha ya Kiswahili. Kwa hiyo, tunakaribisha makala kutoka pande zote za dunia zinazohusu Isimu ya Kiswahili, fasihi ya Kiswahili na utamaduni wa Mswahili.