Hii ni aina ya uanachama kwa wadau wa Kiswahili waishio Afrika. Ukiwa mwanachama hai kupitia aina hii ya uanachama unapata faida zote za uanachama ambazo ni pamoja na:
- Kuunganishwa na wataalamu na wadau wa Kiswahili watokao maeneo mbalimbali duniani
- Kupata punguzo katika majarida na bidhaa mbalimbali za CHAUKIDU
- Kupewa punguzo la ada ya kushiriki Makongamano ya CHAUKIDU
- Kupewa nafasi ya kwanza kuchapisha makala kwenye Jarida la CHAUKIDU
- Ukiwa Mwanafunzi kupewa kiasi fulani cha Ufadhili kuhudhuria Makongamano.
- Kuweza kushiriki katika Warsha mbalimbali.
- Kwa wanafunzi, kuweza kuunganishwa na Walezi, Wataalamu waliobobea katika taaluma mbalimbali za Kiswahili.
- Kupata fursa ya kutangamana na Wapenzi, Watafiti na Wanataaluma za Kiswahili kutoka kote Duniani. Makongamano ya CHAUKIDU huandaliwa katika nchi tofauti kila Mwaka.