Kongamano la Kimataifa la Chaukidu
Nairobi, Kenya
Hisani huanzia nyumbani! Chaukidu kingependa kutangaza kuwa kitakuwa na kongamano la kwanza katika eneo la Afrika Mashariki kikishirikiana na Chuo Kikuu cha Katoliki cha Afrika Mashariki, CHAKAMA na CHAKITA. Mada kuu ni “Taaluma za Kiswahili Karne ya 21 Nyumbani na Ughaibuni: Tutokako, Tulipo, na Tuendako!” Walengwa wakuu wa kongamano ni wanataaluma na wadau wa Kiswahili katika Afrika Mashariki, Afrika na dunia kwa ujumla.
Mahali | Chuo Kikuu Katoliki cha Afrika Mashariki, Nairobi |
Tarehe | Disemba 16 - 17, 2016 (Ijumaa/Jumamosi). |
Kufika | Alhamisi Disemba 15, 2016. |
Ikisiri | Juni 20, 2016 |
Majibu | Julai 11, 2016 |
Miswada | Septemba 30, 2016 |
Tafadhali wasilisha ikisiri yako katika muda uliopangwa. Tuma ikisiri yako kwa: chaukidu2016nairobiconference@gmail.com
Kupata maelezo zaidi kuhusu kongamano hili, chagua katika menyu iliyoko upande wa kushoto wa ukurasa huu