CHAUKIDU secretariat@chaukidu.org

UsajiliZanzibar2018

Usajili na Ada ya Kongamano

Ili kuhudhuria kongamano la CHAUKIDU Disemba 2018 Kisiwani Zanzibar, ni muhimu ujisajili. Tunawahimiza wote mfikirie kujisajili kama wanachama wa CHAUKIDU kwanza kabla ya kujisajili kwa ajili ya kongamano. Unaweza kujisajili mtandaoni kupitia ukurasa wa CHAUKIDU ambao una kiungo cha PayPal. Pia unaweza kujisajili na kulipia ada yako kwa njia za simu. Utaratibu utaletwa kupitia njia mbalimbali za mawasiliano, ikiwemo WhatsApp na barua pepe. Ikiwa haiwezekani kufanya usajili kwa kutumia njia hizo, usajili unaweza kufanywa wakati wa kongamano bila faini.

Warsha

Kutakuwa na warsha ya BURE itakayotolewa siku moja kabla ya kongamano, tarehe 14 Disemba. Warsha hii itatolewa na wataalamu wabobezi katika ufundishaji wa Kiswahili kama lugha ya kigeni Prof. Alwiya Omar kutoka Chuo Kikuu cha Indiana, na Prof. Kiarie Wa'Njogu kutoka chuo Kikuu cha Yale, na Prof. Haroun Maalim kutoka SUZA. Warsha hii itatolewa ikiwa tu watakuwepo watu wenye hitaji hilo. Watu hao watapaswa kujaza fomu ya usajili. Katika fomu hiyo unaombwa kueleza ikiwa una uzoefu wowote wa kufundishaji Kiswahili kama lugha ya kigeni na kuorodhesha vipengele vya ufundhishaji ambavyo ungependa watoa warsha wavigusie. Kujaza fomu ya warsha, tafadhali bofya hapa.

Viwango vya Ada

 Hadhira

Gharama za Usajili

Wanafunzi (Tumia kitambulisho cha chuo)TSh. 50,000 au $25
Washiriki kutoka Barani Afrika TSh.  80,000 au $40.00
Washiriki kutoka nje ya AfrikaTSh. 340,000 au $150.00
  

 

Lipia Usajili Hapa


Gharama za Usajili



Uanachama wa CHAUKIDU
Ili kulipia uanachama wa CHAUKIDU, tafadhali utembelee ukurasa wa CHAUKIDU (chaukidu.org). Tungependa kuwahimiza nyote kujiunga na Chama rasmi. Bofya Hapa Kujiunga na Chama.