CHAUKIDU secretariat@chaukidu.org

Zanzibar 2018

Kongamano la Kimataifa la 4 la Chaukidu

Disemba 15 - 16, 2018 Zanzibar, Tanzania

Chaukidu kingependa kutangaza kongamano la nne la kimataifa na la tatu katika eneo la Afrika Mashariki litakalofanyika katika Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA), Zanzibar Tanzania. Kongamano la nne la Kimataifa litafanyika Zanzibar, Tanzania katika Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA). Kongamano hili linaletwa kwenu na Chaukidu kwa kushirikiana na Idara ya Kiswahili ya Chuo Kikuu cha Zanzibar. Mada kuu ni “Kiswahili na Taaluma Zake Nyumbani na Ughaibuni: Umilikaji, Umilisi, Utumiaji na Utandawazi”. Kongamano hili linalenga kuwaleta pamoja wadau, wazungumzaji, watumiaji na wanataaluma wa Kiswahili kwa ujumla kutoka katika nchi za Afrika Mashariki na Afrika nzima, Marekani, Ulaya na dunia kwa ujumla. 

MahaliChuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar
TareheDisemba 15  - 16, 2018 (Jumamosi na Jumapili)
WarshaIjumaa Disemba 14, 2018
IkisiriMei 31, 2018
MajibuJuni 30, 2018
Miswada Oktoba 30, 2018

 

Tafadhali wasilisha ikisiri yako katika muda uliopangwa. Kupata maelezo zaidi kuhusu kongamano hili, chagua katika menyu iliyoko upande wa kushoto wa ukurasa huu.

Ikiwa ungependa kuchangia kongamano hili, basi unakaribishwa kufanya hivyo. Tuna idadi kubwa ya wanafunzi wa uzamivu na uzamili ambao wangependa kuhudhuria kongamano hili ila wanashindwa kwa sababu ya gharama kubwa. Mchango wako utasaidia kuwafadhili wanafunzi hawa, hasa kwa malazi. Kwa kuchangia, tafadhali tumia kitufe kilichopo hapo chini.

Toa Mchango Wako Hapa